Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima wa pareto Mbeya washauriwa kutovuna ikiwa mbichi

Ofisa pareto kutoka Kampuni ya Pareto Tanzania(PCT) Mkoa wa Mbeya, Mussa Malibano akiangalia ubora wa maua ya pareto katika Kijiji cha Igale Wilaya ya Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Lengo ni kudhibiti tatizo la unyevu ambalo linatokana na uchumaji holela na uhifadhi usio salama wakati wa kusubiri masoko, jambo linalosababisha zao hilo kupoteza sifa na ubora wa kupata masoko.

Mbeya. Wakulima wa zao la pareto katika kijiji cha Igale wilaya ya Mbeya wametakiwa kuacha kuchuma na kuuza maua mabichi yasiyo na ubora, jambo linalosababisha zao hilo kupoteza sifa kutokana na kuathiriwa na unyevu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Septemba 3, 2023, Ofisa Pareto kutoka kampuni ya Pareto Tanzania (PCT), Mussa Malubano amesema kipindi kirefu kumekuwa na changamoto hiyo inayosababisha hasara kwa kampuni kuyahudumia maua katika hatua ya kukausha na kusafirisha kwenda sokoni.

“Unajua wakulima wanapokuwa na uhitaji wa pesa hawasubiri mpaka maua yawe kwenye ubora, hivyo wanalaghaiwa kuchuma na kuuza, lakini pia wana changamoto ya namna ya kuhifadhi kutokana na ukosefu wa mabanio ya kukaushia,” amesema.

Malubano amesema kutokana na hali hiyo, kama kampuni kwa kushirikiana na Taasisi ya Lutheran World Relief (LWR) wameweka mikakati ya kujenga vituo vya mabanio kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuanika maua mara baada ya kuchuma.

Amesema lengo la mpango huo ni kuona maua ya pareto yanazalishwa katika ubora kila msimu, jambo ambalo litasaidia kampuni kurejesha mchango wao kwa kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya na huduma nyingine za msingi.

“Uendeshaji wa kampuni ni kuona faida inapatikana na sio hasara za makusudi na kwamba ili kuepuka hasara hiyo wamefika wakati sasa kutoa elimu kwa mawakala na wakulima kutouza wala kununua maua yasiyokuwa na ubora kwa kuingiza sokoni,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Licha ya changamoto hizo, kampuni imechangia saruji yenye thamani ya Sh300,000 katika shule shikizi ya kata ya Igale kwa lengo la kusaidia wanafunzi wa elimu ya awali kutotembea umbali wa kilometa tano kufuata elimu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi,”amesema.

Naye mkulima wa pareo, Peter Mwambizi amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa jamii na kuomba kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali katika kilimo cha pareto ili waweze kuzalisha kwa ubora na kuchuma maua yaliyo na bora na kiwango kinachostahili.

Mkulima mwingine, Janeth Aloyce amesema elimu ni muhimu kwa wakulima na pia wapatiwe mitaji kwani hilo limekuwa ni changamoto kubwa inayosababisha kuuza maua mabichi ili wajipatie fedha kwa haraka.

“Kwa mfano unakuwa na mahitaji makubwa ya fedha hususan kununua chakula, huku shambani kuna pareto na wanunuzi wapo ni lazima nichume niuze, sasa ili kuweza kukabiliana na hilo wakulima wawezeshwe kiuchumi sambamba na uwepo wa  vifaa vya kukaushia na kutunzia mara baada ya kutoa shambani,” amesema.