Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima, wafanyabiashara wa chai waitwa kuchangamkia fursa mkutano AGRF

Muktasari:

  • Uzalishaji wa zao la chai umeongezeka kutoka tani 24,825 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani 26,754 kwa mwaka 2022/2023 na jumla ya tani 21,091 zimenunuliwa nje ya nchi.

Dodoma. Wakulima wa zao la chai nchini wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa za masoko zitakazotokana na Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF).

Mkurugenzi wa Huduma na Usimamizi, Kemilembe Kafanabo amesema kuwa Bodi ya Chai inaendelea kuhamasisha wazalishaji wa chai kuzingatia matakwa ya vyeti vya ubora (rainforest alliance, sustainable agriculture, Fair Trade na viwango vingine vya kimataifa).

Kafanabo ameeleza kuwa Bodi ya Chai kwa kushirikiana na wadau muhimu imeendelea na maandalizi ya uanzishwaji wa mnada wa chai wa kidigitali utakaokuwa jijini Dar es Salaam.

Vilevile, bodi hiyo inaendelea kusajili wanunuzi wa chai kutoka nje ya nchi ambao wameanza kushiriki katika mnada huo ulioanza shughuli zake mwishoni mwa mwezi Mei, 2023.

Kuhusu vipaumbele vya kuchochea uzalishaji na mauzo ya zao la chai, Kafanabo amefafanua kuwa moja ya kipaumbele kilichowekwa ni kuhamasisha, kusimamia na kudhibiti uzalishaji ili kuongeza ubora wa chai unaokidhi viwango vya soko.

“Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food System Forum) unaleta shauku na hamasa kubwa kwa wazalishaji na wauzaji wa chai kupata taarifa mbalimbali zitakazochochea zao hilo kupata mapato zaidi,” amesema Kafanabo.

Aidha, uzalishaji wa zao la chai umeongezeka kutoka tani 24,825 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani 26,754 kwa mwaka 2022/2023 na jumla ya tani 21,091 zimenunuliwa nje ya nchi, huku vijana na wanawake wakiwa wanufaika zaidi katika ajira zitokanazo na kilimo cha chai.

Mkutano wa Jukwaa la AGRF umepangwa kufanyika Septemba 5,  hadi 8 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam.