Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walimu shule binafsi watakiwa kufichua maovu ya waajiri wao

Muktasari:

  • Kongamano la kitaaluma la walimu wa shule za binafsi Tanzania (TPTU) limefanyika leo Oktoba 8, 2018 jijini Mwanza ambapo Serikali imewaonya wadau hao wa elimu kuzingatia miongozo ya utoaji elimu nchini

Mwanza. Walimu wa shule binafsi wametakiwa kufichua maovu ya shule wanazofanyia kazi ikiwemo mbinu za wizi wa mitihani na kuajiri walimu kutoka nchi jirani bila vibali.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la kitaaluma la Kitaifa la walimu wa shule za binafsi Tanzania (TPTU), kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa  Joyce Ndalichako, leo Oktoba 8, 2018, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Avemaria Semakafu amesema maovu ya wamiliki wa shule za binafsi yanafichwa na walimu.

“Maovu makubwa yanafanyika private (binafsi) na watekelezaji wake ni nyinyi walimu, unakuta mwalimu anafundisha si raia wa Tanzania na hana vibali lakini tukijua mnawatetea mkisema ooh mara huyu ni mwalimu wa dini,” amesema Semakafu 

Pia aliwataka walimu kutokubali kufanya kazi bila mikataba kwa kuwa wanakosesha Serikali kodi na wao kutoingizwa kwenye mifuko ya mafao.

Naye Katibu Tawala msaidizi wa mkoa wa Mwanza anayesghulikia elimu, Michael Ligola aliwasisitiza walimu kufuata taratibu, kanuni na sheria zote kuhakikisha wanatenda haki huku akiwataka wote wenye tabia ya kuiba mitihani kuacha mara moja.

“Mara nyingi tumepata malalamiko hasa shule binafsi kuwa wanaenda kinyume na taratibu zilizowekwa ikiwemo ukaririshwaji wa wanafunzi, endapo itagundulika kuwa kuna shule iwe ya Serikali au taasisi inakaririsha mwanafunzi kisa hajatimiza kigezo cha kuingia kidato kingine bila kibali tutakuchukulia hatua," amesema Ligola.

Naye Katibu Mkuu wa TPTU, Julius Mabala amesema wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya waajiri kutofuata sheria na taratibu ikiwemo kutishia au kuwafukuza kazi walimu wanaojiunga na chama chao.

Amesema waajiri wengi wamekuwa wakiwaachisha kazi walimu wanaojiunga kwenye chama hicho lakini wakifuatilia wanaambiwa ameondolewa kwa kukosa sifa.