Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliopandisha bendera Mlima Kilimanjaro washuka

Muktasari:

Wadau waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa siku sita kwa ajili ya kupandisha bendera katika kilele cha mlima huo kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika wamerejea huku 79 kati ya 150 waliopanda wakifika katika kilele cha mlima huo.

Moshi. Wadau waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa siku sita kwa ajili ya kupandisha bendera katika kilele cha mlima huo kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika wamerejea huku 79 kati ya 150 waliopanda wakifika katika kilele cha mlima huo.

Walianza kupanda mlima huo Disemba 5 mwaka huu ambapo wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, Makamishna wa Tanapa, Tfs pamoja na mashirika mbalimbali walifanikiwa kupanda mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru.

Akizungumza mara baada ya kushuka kiongozi wa msafara huo kutoka JWTZ, Kanali Martine Msumari amesema idadi kubwa ya waliopanda mlima Kilimanjaro walifanikia kufika kilele cha Uhuru ambapo 79 kati ya 150 walifanikiwa kupandisha bendera ya Tanzania katika kilele hicho.

"Jana tulifanikiwa kuweka bendera ya Taifa katika kilele cha mlima Kilimanjaro, wapandaji waliofanikiwa kufika kiele cha Uhuru ni 79 na hii namba imevunja rekodi haijawahi kutokea maana kulikuwa na msongamano kweli kweli pale Uhuru peak," amesema Kanal Msumari

Kanali Msumari ametoa ombi kwa bodi ya wadhamini ya Tanapa kuangalia namna ya kumpa ubalozi wa heshima mtangazaji maarufu wa BBC, Salim Kikeke ambaye alikuwa miongoni mwa waliopanda mlima kuwa balozi wa utalii kutokana na wingi wa watu alionao katika mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Shirika la Hifadhi la Tanzania (Tanapa), Jenerali George Waitara amewapongeza wale wote ambao walifanikiwa kupandisha bendera katika kilele cha Uhuru, Mlima Kilimanjaro na kusema wameonyesha uzalendo mkubwa katika nchi yao.

"Niwapongeze wale wote mliopanda mlima Kilimanjaro na kufika kileleni ,najua mmekuja na simulizi nyingi za kupanda mlima Kilimanjaro tangu mmeanza kupanda mlima wetu  kwa siku zote 6, mmeonyesha uzalendo mkubwa katika nchi yetu na mwaka ujao najua mtakuwa wengi zaidi na tutafungua mageti yote ya kuingilia mlima Kilimanjaro,"amesema Waitara.

Kuhusu ombi la Salim Kikeke kuwa balozi wa utalii amesema ataongea na Waziri wa maliasili na utalii, Dk Damas Ndumbaro ambapo amesema ana uhakika kuwa atamkubalia kuwa balozi na kufanya hivyo kutaongeza idadi ya watalii nchini.

Naye Mkuu wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema ataendelea kuhakikisha mlima Kilimanjaro unakuwa salama kwani umekuwa ukiwanufaisha wanachi wengi na Taifa kwa ujumla kutokana na uwepo wa mlima huo.

"Natoa rai kwa wananchi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi na jitihada za kuhifadhi mlima huu ili haya matunda tunayoyaona sasa hivi vizazi vijavyo viweze pia kuyaona matunda haya ya mlima Kilimanjaro,kwani itakuwa ni lawama kwa kizazi kijacho endapo tutautumia vibaya mlima huu,"amesema Kagaigai