Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliopisha mradi mto Kiwira waanza kufanyiwa tathimini

mafundi wakiendela na ujenzi wa mradi la tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni tano kutoka chanzo cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Mradi huo utawezesha upatikanaji wa lita milioni 117 za maji kwa siku, kunufaisha watu milioni moja.

Mbeya. Wataalamu kutoka kampuni ya uthamini ya Romatus Co Ltd ya Jijini Dar es salaamu, imeanza kufanya tathimini ya maeneo ya wananchi waliopisha mradi wa kimkakati wa maji wa chanzo cha maji cha Mto Kiwira wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuanza utekelezi wa mradi kwa tathimini iliyoanza kufanyika leo Jumatano, Juni 26, 2024 ambayo inafanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Mbeya -Uwsa) na wataalamu wa kampuni ya Romatus.

Kaimu Mkurugenzi wa Mbeya –Uwas, Barnabas Konga akizungumza na Mwananchi Digital leo, amesema; “Tuna imani na kampuni hii itafanya tathimini kwa weledi, lengo ni kuhakikisha mradi unatekelezwa na kukamilika kwa wakati ifikapo Machi 31, mwakani,” amesema Konga.

Amesema utekeleza wa mradi huo unakwenda vizuri, hususani kwenye tenki kubwa lenye uwezo wa kujaza lita milioni tano kwa siku katika eneo la New Forest.

Amesema Mkoa wa Mbeya unakwenda kuandika historia ya kuondokana na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama, hususan kwa wananchi waishio pembezoni mwa mradi utakakopita.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Romatus, Amimu Lusekelo amesema wamejipanga kutekeleza mradi huo kulingana na makubaliano na utakamilika kwa muda uliopangwa.

"Kazi ya uthamishaji wa maeneo inaanza rasmi leo na itadumu kwa mwezi mmoja kuanzia sasa na tutakuwa tumepata takwimu halisi za wananchi watakaopisha mradi huu,” amesema Lusekelo.

Mradi wa maji mto Kiwira utanufaisha watu milioni moja na  utazalisha lita 117 milioni kwa siku na kuwa mwarobaini wa adha ya maji katika Mkoa wa Mbeya na mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi, Wilaya ya Mbeya vijijini.

Mkazi wa Forest Jijini hapa, Sekela Mwakilasa amesema wakati Serikali ikiendelea kupambana na utekelezaji wa mradi huo, isisahau kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto hiyo ya maji inayowakabili wakazi wengi wa mji huo.

Amesema hivi sasa wanaendelea kupata maji kwa mgawo kwa baadhi ya maeneo.

"Kwanza tunaishukuru Mbeya -Uwsa kwa jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na Serikali kuona jamii itafika wakati kuandika historia ya tatizo la maji, lakini wakati mradi huo ukiendelea uwekwe utaratibu wa kusaidia maeneo yenye changamoto,” amesema.