Wanachama 49 wachukua fomu kuutaka uspika

Katibu Mkuu msaidizi CCM Solomon Itunda

Muktasari:

Ikiwa zimebaki siku mbili kufungwa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, wanachama 49 wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo mpaka leo Alhamisi Januari 13, 2022.

Dodoma. Ikiwa zimebaki siku mbili kufungwa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, wanachama 49 wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo mpaka leo Alhamisi Januari 13, 2022.

Katibu msaidizi Mkuu idara ya Oganaizesheni Solomon Itunda amewaambia waandishi wa habari leo kuwa wanachama 19 wamejitokeza leo kuchukua fomu hizo hivyo kufanya jumla ya waliochukuwa kufikia 49 ambapo hadi jana juoni walikuwa wanachama 30 walikuwa wameshachukua.

Leo waliochukua kwa Ofisi ya Dodoma walikuwa 9 wakati Ofisi ya Dar es Salaam walikuwa 10.

Itunda amewataja waliochukua Ofisi ya Dodoma ni Ezekiel Maige, Emmanuel Mng'arwe, Azizi Mussa, Onyango Otieno, Dotto Mgasa, Profesa Edson Lubua, Fikiria Said, Dk Itikija Mwanga na Peter Njemu.

Kwa Ofisi ya Dar es Salaam ni Ndurumah, Majembe, Godwin Maimu, Johnson Japheth, Mohamed Manga na Ester Makazi.

Wengine ni Mariam Koja, Joseph Anania, Samuel Xsaday, Arnold Peter na Joseph Sabuka huku Ofisi kuu ya Zanzibar haikuwa na mtu aliyechukua Kwa siku ya leo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wanachama wanaombwa kutumia siku mbili hizi kati ya kesho na kesho kutwa kukamilisha mchakato huo kwani chama kinaanini haki itatendeka na anayestahiki atapewa.