Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi 12,000 hatarini kupata magonjwa ya mlipuko

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Thomas Salala(aliyevaa miwani)akiwa na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Chemchem wakifanya usafi katika chanzo cha maji kinachosaidia kata ya Kitere na baadhi ya vijiji mkoani Lindi. Florence Sanawa

Muktasari:

  • Zaidi ya wananchi 12,000 wa vijiji vitano vya Kata ya Kitere Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wako hatarini kupata magonjwa ya kuhara na kutapika yatokanayo na kuchafua chanzo cha maji  ambacho wamekuwa  wakikitumia kwa kuoga na kwa kujisaidia kando ya chanzo hicho huku wakikigeuza kuwa dampo.

Mtwara. Wakazi wa vijiji vitano vya Chemchem, Chekeleni, Lilido, Kitere na Nakada wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko  kutokana na kugeuza chanzo cha maji kuwa choo na dampo.

Akizungumza na Mwananchi ilipotembelea chanzo hicho, Fatuma Mohamed mkazi wa Kijiji cha Chemchem, Kata ya Kitere alisema kuwa wananchi wamekuwa wakaidi hata wanapoambiwa kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji wanaishi kwa mazoea.

“Yaani wananchi hawaelewi na hawasikii unakuta mtu ni mtu mzima kabisa lakini anatoka nyumbani kwake hadi hapa kuja kuoga na anakaa pembeni anajisaidia. Watu wanapuuza hata tukiwaambia hawatuelewi. Sisi hatupendi na hatuvutiwi kabisaa na hii tabia  kwasasabu hivi vinyesi vinatutia kinyaa sisi tunakelekwa na hatupendi kabisaa,” amesema.

kwa upande wake Mratibu wa Vyombo vya Huduma vya Watoa Maji Ngazi ya Jamii kutoka Ruwasa Emmanuel Mwakajila alisema kuwa chanzo cha maji jamii imeanza kukitumia vibaya.

Alisema kuwa matumizi hayo mabaya yamesababisha hadi vinyesi kuwa kando ya chanzo cha maji hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao yaani wamegoma kabisa kusikiliza elimu tunayowapa.

“Unajua wakazi wa vijiji vya Chemchem, Chekeleni, Lilido, Kitere na Nakada yaani wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko ya kuhara na kutapika kutokana na chanzo hichi kumevamiwa na wananchi na kusababisha kuwepo kwa uchafu ambao hata ukiwa karibu, hukimbilia kwenye maji hii inahatarisha afya zao,” amesema.

kwa upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Thomas Salala alisema kuwa kitendo kinacho fanyika katika chanzo hicho ni kinyume cha sheria.

“Nadhani kuna sehemu tumekosea haiwezekani kwenye eneo moja watu wakawa kwenye utaratibu wao na watu tukakaa kimya kwenye hili tunakiri udhaifu, ombi langu kwenu mitazamo yenu ibadilike kuanzia sasa yawezekana kauli nyingi mmesikia lakini kwenye hili tutasimama kidete hatuhitaji kukimbizana wala kufukuzana,” amesema.

“Hivi mnajua kuwa wapo waliotunza chanzo hiki mpaka mkakikuta hivi hata thamani yake hatujui sasa leo naelekeza mtendaji wa kata na timu yake  nikikuta hali hii  tena kuanzia afisa tarafa, mtawajibika kuliko hata mlivyodhani. Hii tabia ikome, nimeshika kinyesi kusafisha chanzo cha maji ambayo mnatumia nyie haya ni matumizi mabaya hii ni rasimalia ya taifa huwezi kusema ni yako haiwezekani,” amesema.