Wananchi manispaa ya Moshi waonywa ukataji wa miti

Wananchi manispaa ya Moshi waonywa ukataji wa miti

Muktasari:

  • Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu  amewaonya  wananchi kukata miti  bila kufuata taratibu  na   watakaobainika kuikata bila kuwa na vibali maalum watakamatwa.



Moshi. Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu  amewaonya  wananchi kukata miti  bila kufuata taratibu  na   watakaobainika kuikata bila kuwa na vibali maalum watakamatwa.

Raibu ameyasema hayo leo Jumanne Septemba 14, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema,  "wapo  baadhi ya watu kwa nia ovu wameendelea kukata miti ovyo ndani ya manispaa ya Moshi na tuliweka utaratibu mzuri na sheria ndogo ili  kuwabana,   miti ikiwepo inasaidia kuendelea kuwepo kwa uoto wa asili."

‘Tunayo haki ya kukata miti lakini tufuate taratibu na  tuombe vibali maana mti ule  ukishaupanda ni wa kwako lakini ukishaota sio wa kwako ni mti wa halmashauri na juzi niliongea na TFS kuna watu walikuwa wanakata miti ovyo eneo la Longuo na wamekamatwa."

“Niwaombe wananchi wangu wa Manispaa ya Moshi kwamba  unapotaka kukata mti njoo kwa mkuu wa Wilaya ,Halmashauriau watendaji wa kata  watakupa taratibu za kufuata ikiwemo kufika kwenye eneo lako na kukagua kasha utapewa kibali cha kukata au la,”

“Ukikata mti bila kufuata taratibu ni kosa natutakukamata na tutakukamata na kukufikisha kwenye vyombo vya sharia kujibu tuhuma zako,:amesema Raibu