Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi Moshi wajitokeza kumpokea Rais

Wananchi Moshi wajitokeza kumpokea Rais

Muktasari:

  • Wakazi wa Wilaya ya Siha wamejitokeza kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan katika eneo la Duch Kona, Kijiji cha Wiri kilichopo katika wilaya hiyo Mkoani Kilimanjaro.


Siha. Wakazi wa Wilaya ya Siha wamejitokeza kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan katika eneo la Duch Kona, Kijiji cha Wiri kilichopo katika wilaya hiyo Mkoani Kilimanjaro.

Wakazi hao wamejitokeza asubuhi leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 ambapo Rais Samia yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Katika ziara hiyo Rais Samia atazindua miradi, kuweka mawe ya msingi na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Samia atazindua barabara ya lami ya Sanya Juu- Elerai yenye urefu wa kilomita 32 iliyogharimu zaidi ya Sh60 bilioni na kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi ambayo inatarajiwa kugharimu Sh12 bilioni hadi kukamilika.

Rais ataweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Rau ambalo lilisombwa na maji ya mvua mwaka juzi, linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh900 milioni.

Atashiriki jubilee ya miaka 50, ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).