Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wafurika kujiandikisha mbolea ya ruzuku

Muktasari:

  • Wakulima wasotea kujiandikisha kupata mbolea ya ruzuku huku waandikishaji wakizidiwa na idadi ya watu.

Songwe. Kuandikisha wanufaika wa Mbolea ya ruzuku lililoanza mapema jana Jumatano Agosti 18, 2022 limeingia dosali ikiwamo uandikishaji kuwa wataratibu unaofanya watu kukaa muda mrefu kwenye foleni.

Mmoja wa wanufaika kutoka Kijiji Cha Oldvwawa, Jailos Kayange amesema utaratibu wa kuandikisha ni mgumu kwani muda uliowekwa wa siku moja kila kijiji hautoshi huku kukiwa na kalani mwandikishaji mmoja ambaye anashindwa kumudu idadi ya watu waliojitokeza.

" Tunapata usumbufu mkubwa kwani Kalani mwandikishaji amezidiwa kuandikisha kwani wakulima kutoka vitongoji 8 na wengine kutoka maeneo mengine ambao wanalima katika Kijiji hicho wameongeza idadi," amesema Kayange

Naye Alfeyo Sichizwa amesema baadhi ya Wakulima jana walikata tamaa kufuatia foleni ndefu ambayo inaenda taratibu na watu ni wengi na kuwa hali hii inachangiwa na wakulima kutakiwa kwenda kujiandikisha maeneo yalipo mashamba yao na si katika maeneo yao ya makazi.

"Ameletwa kalani mmoja ambaye tulikuwa naye tangu jana kalani huyo amezidiwa maana idadi ya watu ni kubwa sana," amesema Sichizwa.

Mwenyekiti wa kitongoji Cha Oldvwawa John Kaminyoge amesema wamepewa kitabu kimoja kata nzima ambacho kinatumika kuandikisha wanufaika ambapo imepangwa kila kijiji ndani ya kata kinaandikisha siku moja.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mbolea nchini (TFRA), Stephen Ngailo Akizungumza na gazeti hili Kwa njia ya simu amewaondoa hofu wakulima kuwa zoezi hilo ni endelevu na kuwa wamelianza mapema Ili kuwafikia wakulima wengi.

"Niwaondoe hofu wakulima zoezi ni endelevu kila mmoja ataandikishwa, tulitoa kitabu kimoja kila kata kwa majaribio tunatarajia kuongeza kwani vitabu vipo vya kutosha," amesema Ngailo.