Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wafurika Uwanja wa Uhuru kumuaga Magufuli

Wananchi wafurika Uwanja wa Uhuru kumuaga Magufuli

Muktasari:

  • Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na mikoa jirani wameendelea kumiminika katika uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano John Magufuli.

Dar es Salaam. Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na mikoa jirani wameendelea kumiminika katika uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano John Magufuli.

Kufikia saa 3:30 uwanja huo ulikuwa umefurika kiasi cha kutolewa matangazo ya kusitisha kwa muda walio nje kuingia ndani.

Pamoja na uwanja kufurika bado nje ya uwanja kulikuwa na watu wengi waliojipanga kwenye foleni ya kutaka kuingia ndani kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe alilazimika kuingia kati na kuwasihi wakazi waliojitokeza kuwa watulivu.

“Tunashukuru kwa namna mlivyojitoa kuja kumuaga baba yetu, nawahakikishia wote mtapata nafasi ya kuaga ila tufuate utaratibu.

Tutahakikisha wote mnamuona na mnatoa heshima, naomba mlio jukwaani msishuke tulieni tufuate utaratibu, lengo tumalize hili bila mtu kuumia,” amesema Gondwe.

Mkuu huyo wa wilaya aliomba pia msaada wa Kamanda wa Polisi wa Temeke kuongeza askari uwanjani hapo ili kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kwa amani.

Askari waliokuwa karibu na jeneza lililohifadhi mwili wa Magufuli walihakikisha kila aliyepita hapo alipata fursa kuona ikiwa ni pamoja na kuwanyanyua watoto ili waweze kumuona hayati Magufuli kwa mara ya mwisho.