Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wachukuliwe hatua kali

Baaddhi ya waumini wa dini ya Kiislaam mkoa wa Katavi wakiswali swala ya Eid El-Fitri leo Jumamosi Aprili 19, 2023 katika viwanja wa Kashato mjini Mpanda. Picha na Mary Clemence

Muktasari:

  • Waumini wa dini ya Kiislaam mkoani Katavi wamesherehekea sikukuu ya Eid el Fitri kwa kupinga mapenzi ya jinsia moja, wakitaka kuchukuliwa hatua kali.

Katavi. Waumini wa dini ya Kiislaam mkoani Katavi wamesherehekea sikukuu ya Eid el Fitri kwa kuunga mkono mapendekezo ya baadhi ya Wabunge ya kutunga sheria kali zitazowawajibisha watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Sheikh wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu akiwahutubia waumini wa dini hiyo leo Aprili 22, 2023 katika viwanja wa Kashato mjini Mpanda amesema wamekubaliana kwa pamoja kuunga mkono hoja na wafungwe miaka 30 jela.

Kama hiyo haitoshi, amesema wanaiomba serikali itunge sheria nyingine kali kwa ajili ya kutokomeza janga hilo huku wakiwapongeza Wabunge waliosimama kidedea kulishawishi bunge kutunga sheria hiyo.

“Ndugu zangu Waislaamu vitabu vyote vya Mungu vimeelezea majanga haya na athari zake na adhabu gani wanazostahili kupata watu wanaoshughulika na mapenzi ya jinsia moja.

“Sisi katika vitabu vyetu vya Quran na katika vitabu vya dini nyingine nadhani pia lipo hilo, kama walivyosema Wabunge wakipatikana mashoga wauawe,” amesema Kakulukulu

Aidha amesema vita dhidi ya mapenzi ya jinsia moja siyo ya serikali au viongozi wa dini pekee bali ni ya jamii nzima hivyo hivyo washirikiane kulaani, kukemea na kupinga vitendo hivyo.

“Kama walivyoomba baadhi ya Wabunge kupima na sisi viongozi wa dini tupo tayari kupimwa ili idhihirike nani anahusika, kwa sababu suala hili linawaangamiza vijana baadaye litarudi kwa wazee hali mbaya sana,” amesema.

Nay Hamisa Saburi amesema vitendo hivyo vinasababishwa na vijana kujiunga katika vikundi viovu vinavyopelekea kuvuta bangi na kutumia dawa za lulevya.