Wanawake 3000 kuchunguzwa saratani bure

Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay

Muktasari:

Akizungumza leo Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay amesema huduma hiyo itatolewa kwa siku tatu kuanzia Jumatano ijayo.

Dar es Salaam. Wanawake zaidi ya 3000 watapata huduma bure ya uchunguzi na matibabu ya saratani ya shingo ya uzazi yatakayotolewa na hospitali za Marie Stopes Tanzania.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay amesema huduma hiyo itatolewa kwa siku tatu kuanzia Jumatano ijayo.

Amesema wanawake wanaohitaji huduma hiyo watatakiwa kufika kwenye hospitali hizo ambazo ziko kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Amesema huduma hiyo itatolewa bure ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 tangu hospitali hizo duniani.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonyesha asilimia 10 ya wanawake duniani wana dalili za ugonjwa huo.