Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake na vijana wapewa mbinu ya kujiingizia kipato

Muktasari:

  • Wanawake na vijana wahimizwa kujikita kwenye mafunzo ya ujasiriamali kama mbinu ya kuingiza kipata na  kukabiliana na ugumu wa maisha.

Dar es Salaam. Bado Vijana na Wanawake nchini wameshauriwa mbinu sahihi ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira ni  kuendelea kujifunza ujasiriamali kwa kupata ujuzi tofauti na kuutumia kuwasidia ili uwe mkombozi katika kujiingizia kipato.

Hayo yalibainishwa Dar es Salaam Mei17, 2025 na Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Orchid Organization, Nasra Pendo kwenye hafla ya kutunuku vyeti vya mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali iliyoandaa kwa wanawake 40 kati yao15 mafunzo ya keki na 25 kutengeneza nguo za batiki.

"Tatizo la ajira ni kubwa vijana wasilale umaskini unachosha, wajitahidi kushiriki mafunzo ya ujasiriamali kwani hata taasisi yetu dhamira yake ni kuwainua wanawake na vijana ni wakati wao kujitokeza," amesema Nasra

Kwa upande wake Katibu wa taasisi hiyo, Lilian Mtundu amesema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali kwa wanawake na vijana ikiwemo kutengeneza keki na nguo aina ya batiki.

"Tuna mwaka mmoja tangu tulipoanzisha taasisi na tumekuwa tukisaidia kundi hili na kuna wanaotengeneza keki na batiki wakinufaika na mafunzo tunayotoa na katika masoko tunawaunganisha na wadau mbalimbali," amesema Lilian

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Dorah Nntemo ameishukuru taasisi hiyo kwa mafunzo hayo kwani kwa sasa anajua kutengeneza keki na batiki na kujipatia kipato.

"Tofauti na mwanzo nilikuwa nakaa bure muda mwingi nyumbani si kuwa na kazi ya kufanya lakini sasa najivunia ujuzi niliopata manufaa naanza kuyaona nawashauri na wengine wasipuuze mafunzo," amesema Dorah

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, (CCM) Kata ya  Msigani, Winfrida Muhiji  amehitimu hao kuongeza bidii katika kendelea kushiriki mafunzo yanayochochea kuwa na ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbalimbali ili kuinua maisha yao.

"Msidharau mafunzo msikate tamaa ukiwa na ujuzi hata kutengeneza batiki tengeneza nenda kauze hata huko mkoani kuna soko, biashara ndogondogo ndizo zinainua wanawake kiuchumi," amesema

Kwa upande wake,Mbunge wa Kibamba,Issa Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi, ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya huku akiahidi kuiunga mkono ili ifike mbali zaidi.

"Mmeniomba niwaunganishe na taasisi mbalimbali hilo halina shida ndiyo kazi ya mbunge nitafanya hilo msiwe na wasiwasi na mahitaji yenu mengine yaandikeni vizuri nileteeni niyaangalie nijue namna ya kuwasaidia," amesema Mtemvu.