Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake waishauri Serikali kuhusu ukatili wa kijinsia

Muktasari:

  • Mtandao  wa wanawake wa dini mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria  zinazochochea ukatili wa kijinsia ikiwemo  masuala ya mirathi na ndoa za utotoni.



Moshi. Mtandao  wa wanawake wa dini mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria  zinazochochea ukatili wa kijinsia ikiwemo  masuala ya mirathi na ndoa za utotoni.

Wameyasema hayo walipokutana mjini Moshi  katika mkutano ulioandaliwa na makao makuu ya Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (ELCT), Dayosisi ya Kaskazini kwa ushirikiano na Norwegian Church Aid Tanzania.

Mwenyekiti wa wanawake wa dini ya  kiisalmu mkoani Kilimanjaro, Zawia Massawe amesema ni wakati sasa Serikali kupitia wizara husika kuona umuhimu wa kufanya marekebisho hayo ya kisheria zinazokandamiza haki za kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike.

“Kuna vitu  vinachochea ukatili wa kijinsia kwenye jamii zetu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa baadhi ya sheria zisizo rafiki katika kudhibiti vitendo hivi  na zinapaswa kutazamwa upya, tunaomba Serikali iangalie hili kwa jicho pana,” amesema

Pamoja  na mambo mengine, Josephine Shoo ambaye ni kiongozi wa wanawake katika makanisa ya kipentekoste ameiomba Serikali  kushirikiana na wadau wengine kutenga rasilimali za kutosha kuchangia mambo  yanayohusu afya bora na usawa wa kijinsia.