Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne mbaroni tuhuma ya kumteka mtoto Katavi, wakitaka Sh50 milioni ili kumuachia

Katavi. Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma  za  kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda Manispaa ya Mpanda, kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja wakitishia kumuua huku wakihitaji Sh50 milioni ili wamwachie.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amewataja watuhumiwa hao waliohusika na tukio hilo kuwa ni  Joseph  John(24), Yusuph  Sadick  (27) wakazi wa Mtaa wa Milupwa , Abrahamu  Kassim(28) Mkazi wa Mtaa wa Misunkumilo na Samwel Nzobe (41) mkazi wa Mtaa wa Kotasi.

Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa ya kutekwa kwa mtoto huyo.

Kamanda Ngonyani amesema kuwa  tukio hilo la kikatili  limetokea  June 13,2023  saa  8 kamili mchana  katika Manispaa ya Mpanda wakati mtoto huyo alipokuwa anarudi shuleni kufanya usafi.

Ameeleza kuwa wakati akiwa njiani  jirani na Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda watuhumiwa hao wanne walimteka  mtoto huyo na kumpeleka kusikojulikana  kisha  kumtishia kumuua au walipwe na  mzazi wake kiasi hicho cha Sh50 milioni ili wamuache akiwa hai.

Amesema  Juni  14, 2023 polisi walifanikiwa kumpata mtoto huyo akiwa salama katika maeneo ya Mtaa wa Milupwa Manispaa ya Mpanda  akiwa amefichwa ndani ya chumba  cha mtuhumiwa  Joseph John.

Amesema watuhumiwa  wote  wanaendelea  kushikiliwa na jeshi la polisi  kwa mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo  mara  baada ya upelelezi  kukamilika watafikishwa  mahakamani  kujibu tuhuma zinazo wakabili.