Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne wafariki kwa kuangukiwa na ukuta kanisani, 12 walazwa Dodoma

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Kijiji cha Wiliko, Gabriel Mika amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza sababu kwamba ilitokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Dodoma. Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa Kanisa.

Tukio hilo limetokea jioni ya Jumatano Desemba 23, 2025 katika Kijiji cha Wiliko Kata ya Mlowa Wilaya ya Chamwino ambapo Ukuta wa Kanisa la Anglikana ulianguka wakati waumini wakiwa ndani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Dodoma, Gallus Hyera hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani mara kadhaa simu yake ilipopigiwa haikuwa hewani.

Samson Kabohola akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo mke wake ni mmoja wa waliofariki.

Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk Dickson Chilongani ametangaza michango kwa makanisa yote kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi hao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Wiliko Gabriel Mika amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza sababu kwamba ilitokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ambapo watu 17 walijeruhiwa na wengine watano kupatiwa matibabu katika zahanati ya kijijini hapo, huku 12 wakipelekwa hospitali ya mjini Dodoma.

"Ni kweli amefariki mwanaume mmoja na Wanawake watatu wote ni watu wazima wa kijijini kwangu, hapa nipo msibani," amesema Mika.

Amesema siku ya Jumatano majina ya mchana kulikuwa na ibada ya ubatizo na ushirika ambapo waumini wengi walikusanyika kanisani hapo na wakati ibada ilipofika mwisho, ilishuka mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

"Mchungaji aliwaomba waumini kurudi majumbani lakini wengi wakaona heri wajifiche hapo ndipo ukaanguka ukuta wa jengo hilo, eneo la tukio tulimpoteza watu wawili na hawa wawili walifia hospitali kabla ya kupata matibabu," amesema Mika.

Neema Bwanga mmoja wa majeruhi akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti, majeruhi walikuwa 17 ambapo baada ya wawili kupoteza maisha, walibaki watano wanaoendelea kutibiwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dk Ernest Ibenzi amekiri kupokea majeruhi 12 wa tukio hilo ambao amesema wanaendelea na matibabu.

"Sisi tulipokea majeruhi 12 kutoka katika tukio hilo, tunashukuru Mungu kwamba wote wanaendelea vizuri na matibabu hapa Hospitali na hatuna kingine tofauti tangu walipoletwa hapa," amesema Ibenzi.

Mmoja wa majeruhi ambaye ni mzee wa Kanisa hilo Neema Bwanga amesimulia mkasa mzima akisema ulianza upepo ambao ulitikisa na kuangusha vikombe vya ushirika.

Amesema baada ya hapo hajui kilichotokea badala yake amepata fahamu akiwa hospitalini na kukiona akiwa na wenzake.