Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanyama wakali watishia makarani wa sensa Monduli

Muktasari:

  • Zikiwa zimebaki siku mbili pekee kuhitimisha sensa ya watu na makazi kote nchini, wanyama wakali wametajwa kuwa tishio la makarani wanaofanya kazi hiyo wilayani hapa.


Monduli. Zikiwa zimebaki siku mbili pekee kuhitimisha sensa ya watu na makazi kote nchini, wanyama wakali wametajwa kuwa tishio la makarani wanaofanya kazi hiyo wilayani hapa.

Akizungumzia hali hiyo leo Agosti 27, Mkuu wa wilaya hiyo, Monduli Frank Mwaisumbe amesema kuwa wilaya yake imefikia asilimia 81 ya uhesabuji wa kaya zilizoko katika Eneo lake huku changamoto ya Wanyama ikiwa kikwazo kikubwa.

"Uzururaji wa tembo, nyati na chui umekuwa tishio kwa makarani wetu, hali ambayo inawalazimu kusimama eneo moja kwa muda mrefu kuwasiliana na kuwasusubiri maafisa Wanyama pori pindi tu wanapowaona hivyo kuchelewesha zoezi zima," amesema.

Mwaisumbe alisema changamoto nyingine ni kaya kuwa mbali mbali hivyo kuchukua mda mrefu kwa karani kutoka kaya moja kwenda nyingine kwa miguu kukamilisha kazi kutokana na baadhi ya maeneo kutokuwa na miundo mbinu ya kufaa kwa usafiri.

"Mbali na hayo wilaya yetu Ina changamoto kubwa ya umeme hivyo makarani kulazimika kukatiza kazi endapo kishkwambi chake kinapoisha chaji, na kwenda eneo la mji kutafuta nishati hiyo," alisema Mwaisumbe

Mkuu hiyo amesema kuwa, katika kukabiliana na changamoto hizo, wameweka vituo vingi vya kusimama maafisa wanyama pori wakiwa na magari yao ili kurahisisha kazi pindi tu wanapopigiwa simu ya kuhitajika msaada ya kuwaokoa makarani dhidi ya Wanyama wakali.

"Tumeweka pia magari yenye uwezo wa kusaidia kuchaji vishkwambi hivyo pindi vinapoisha chaji, yote hii ni kusaidia kazi iende kama ilivyopangwa ambapo tunakimbizana nayo kuhakikisha ndani ya hizi siku mbili zilizobaki kaya zote za wilaya yetu ziwe zimefikiwa," amesema.

Mmoja wa wakazi wa eneo la Mbuyuni, Saruni Ezekieli ameiomba Serikali kuwasaidia makarani wa sensa kuwafikia wananchi wote ili kupata huduma muhimu za kijamii.

"Eneo letu lina uhaba mkubwa wa maji, pia miundo mbinu ya umeme hakuna na zaidi hospital pia kwetu hakuna hivyo tunaogopa tusipofikiwa na sensa hatutapata huduma hizo kutoka Serikalini," amesema. 

Naye ofisa wa sensa wilaya ya Monduli, Ngakoka amesema makarani wao wanaendelea vema na kazi waliyopewa na hadi siku ya mwisho wanatarajia watakamilisha kazi nzima ili kuhakikisha wanaisadia Serikali kupanga mipango ya maendeleo.