Washtakiwa wanne mauaji ya Alphonce Mawazo kujibu kesi

Washtakiwa wanne mauaji ya Alphonce Mawazo kujibu kesi

Muktasari:

Miaka mitano tangu kuuawa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa na mgombe aubunge Jimbo la Busanda, Alphonce Mawazo, watuhumiwa wanne wamekutwa na hatia ya kujibu.

Geita. Washtakiwa wanne kati ya watano wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa  Chadema Mkoa wa Geita na Kanda ya Ziwa, Alphonce Mawazo, wamekutwa na kesi ya kujibu.

Waliokutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ni Alfan Apolnari, Epafra Zakaria, Hashim Sharifu na Kalulinda Bwire.

Mawazo aliuawa siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Katika uchaguzi huo Mawazo aligombea ubunge jimbo la Busanda..

Katika shauri hilo namba tisa la mwaka 2019, mshatakiwa wa nne, Habibu Feruzi ameachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kushindwa kuthibitisha kuhusika kwake kwenye mauaji hayo ya kukusudia hivyo kutokuwa na kesi ya kujibu.

Hakimu mwandamizi mwenye mamlaka ya juu kusikiliza kesi ya mauaji, Frank Mahimbali ameieleza mahakama kuwa baada ya kuitafakari kesi yote na kusikiliza upande wa mashtaka na mashahidi 13 pamoja na vielelezo vitano na ushahidi, mahakama imewakuta na kesi ya kujibu washtakiwa wanne.

Mahimbila amesema hayo aliposikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita