Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataalamu wa fedha wanolewa matumizi ya Tehama

Muktasari:

  • Wataalamu wa maswala ya fedha nchini wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kupatiwa elimu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuleta ufanisi zaidi kazini.

Arusha. Wataalamu wa maswala ya fedha nchini wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kupatiwa elimu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuleta ufanisi zaidi kazini.

Mkutano huo wa siku tatu  unahusisha Wataalamu zaidi ya 400 wa maswala ya kifedha kutoka taasisi mbali mbali za kifedha zikiwemo mabenki, wahasibu, wakaguzi, maofisa wa bima na mapato.

Akizungumzia malengo ya mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania, Pius Maneno amesema wanalenga kuwaelimisha zaidi wataalam hao juu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma ambayo ni rahisi na yenye ufanisi zaidi ili kuendana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda.

"Hapa tuna mada 11 tunazo elekezana zaidi ni matumizi ya mtandao katika kutoa huduma zetu za kifedha ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi za kifedha na namna ya kuzuia viatarishi vya kuzuia malengo yetu" alisema Maneno.

Maneno alisema kuwa wanatarajia pia kuwanoa washiriki wao katika kutambua mbinu za masoko ya kazi zao, maswala ya Kodi, utawala Bora, jinsi ya kuandaa na kuandika taarifa za kuripoti maswala ya fedha lakini pia kukumbushana majukumu ya wahasibu na Benki Kat utoaji wa taarifa za fedha haramu zinapojitokeza.

"Lengo la haya yote ni kufanya wataalam wetu wajue majukumu yao, lakini kutumia Tehama katika kuhudumia jamii ambayo itarahisisha kazi na itawafikia wananchi wengi kwa bei nafuu na itapunguza umaskini kwa kukuza uchumi", alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Arusha, Çharles Yamo alisema kuwa mafunzo hayo wamekuwa wakiyatoa ili kuwafanya wataalamu hao waendane na kasi ya dunia kwenye mapinduzi yaliyopo katika utoaji wa huduma za kifedha.

"Katika mkutano huu jambo kubwa ni mapinduzi ya nne ya viwanda katika matumizi ya  Tehama, katika ukuaji wa  uchumi wa jamii na nchi na nchi kwa ujumla wake"

Alisema kuwa wanasisitiza pia maadili katika utoaji wa huduma na wahusika wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za mikopo yao na riba lakini pia wakopaji katika taasisi zao ili kupunguza tatizo la mikopo chechefu.

"Tunawasisitiza pia taaisis wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za wakopaji wao ili zisaidia taasisi zingine kuzipata na kutumia dhidi ya wateja wanaokwenda kukopa pengine na kujiridhisha endapo mkopo huo hautawaathiri, hiii itasaidia kupunguza mikopo chechefu kwa wateja lakini pia heshima kwa Benki"


Yamo alitumia nafasi hiyo kuwaonya taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo mitaani bila leseni ya kufanya biashara hiyo wala kibali cha BOT kuwa watawachukulia sheria.

"Pia niwaombe mabenki watoa mikopo kwa riba elekezi ya Serikali isiyozidi asilimia 15 kwa mikopo mikubwa ya mda mrefu Hadi asilimia saba ili kuleta maana ya kuwasaidia wananchi wakopaji na sio kuwakandamiza"