Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataalamu wa lishe waonya matumizi ya chumvi nyingi

Muktasari:

  • Baadhi ya wataalamu wa lishe nchini wameonya juu ya tabia ya matumizi ya chumvi ya mezani, kwani husababisha magonjwa yakiwemo ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Dar es Salaam. Baadhi ya wataalamu wa lishe nchini wameonya juu ya tabia ya matumizi ya chumvi ya mezani, wakisema ni jambo la hatari, kwani husababisha magonjwa yakiwemo ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

 Wadau hao wamebainisha hayo leo Februari 21, 2023 wakati wa mjadala wa Mwananchi Twitter Space uliokuwa na mada inayohusu “Jinsi ya kuepuka magonjwa yasababishwayo na matumizi chumvi ya mezani.”

Akizungumza katika mjadala huo, mtaalamu wa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO), Stella Kimambo amesema limekuwa ni jambo la kawaida kukuta chumvi mezani na mtu anaongeza kabla hata ya kuonja chakula kubaini kama kina chumvi au la.

“Sasa hivi kila meza katika hoteli au mgahawa utaona kuna vikopo vya vya chumvi, kuna tabia ya kuongeza chumvi bila hata kuonja chakula, sio jambo jema.

“Hata katika nyumbani watu wana tabia kabla ya kuonja chakula wanaongeza chumvi,” amesema Kimambo.

Amesema chumvi iliyoongezwa madini joto ndiyo inayotakiwa kutumia na watu wanaweza kuibani kwa sababu imeandikwa kwenye pakiti yake. Amesisitiza kwamba chumvi imekuwa tishio kwa afya za watu.

“Tabia ya kuongeza chumvi katika chakula inatuletea mzigo mkubwa katika taifa letu,” amesema mtaalamu huyo wa lishe.

Kwa upande wake, Paul James amesema namna ya kuepuka na magonjwa yanayosababisha na chumvi ya mezani, lazima elimu itolewe kwa watu wa kawaida kuanzia wazazi na ndugu ambao wana tabia ya kuongeza chumvi.

“Vyombo vya habari na wanataaluma mbalimbali kueleza haya katika ngazi mbalimbali kuhusu matumizi ya chumvi ya mezani. Pia wanafunzi wanatakiwa kuambiwa kuhusu matumizi ya chumvi.

“Sasa wakieleza hayo ule utamaduni wa watu kuongeza chumvi wataacha, pia kuwepo na mpango wa kuondoa tabia hii. Kama ni hoteli mmetengeza hatua za kukabiliana na matumizi ya chumvi ya mezani, hata watoa wa huduma za chakula wanapaswa kupewa elimu hii,” amesema.