Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataka Polisi kukomesha mauaji Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa.

Muktasari:

  • Wakazi wa mji wa Songe na vitongoji vyake wapo katika hofu baada ya kutokea mauaji ya kikatili ya mfululizo yakiwamo ya bodaboda aliyekutwa mikono na miguu.

Kilindi. Hofu imetanda kwa wakazi wa Mji wa Songe na vijiji jirani kufuatia matukio ya mauaji ya kikatili yanayodaiwa kutokea mfululizo, likiwamo la dereva wa bodaboda ambaye mwili wake ulikuwa ukiwa hauna viganja vya mikono na miguu.

 Kufuatia matukio hayo, wananchi hao wamemuambia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga kuendesha msako utakaowezesha kukamatwa kwa wauaji hao ambao wanatushia uhai wa wananchi.

Kwa mujibu wa habari zilizotufukia na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa ni kuwa kwa kipindi cha wiki mbili wameuawa watu watano katika matukio tofauti.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Kilindi, Diwani wa Kata ya Songe, Mohamed Makengwa aliwataja waliouawa ndani ya wiki mbili kikatili kuwa ni dereva wa bodaboda aliyepotea Oktoba 10 mwaka huu na mwili wake kukutwa eneo la Mnara nje kidogo ya Mji wa Songe.

"Huyu bodaboda alipotea tangu Oktoba 10 tukaanza kumtafuta, jana wenzake wakaona kikaratasi chenye ujumbe unaoeleza kuwa mkamuokote Abdallah mnarani...kwa kweli kauawa kikatili sana, hana viganja vya mikono na miguu vyote vimekatwa," amesema Makengwa.

Amemtaja mwingine kuwa ni Juma Issa Lukuni aliyekutwa ameuawa katika mazingira yenye utata na mwili wake kutupwa eneo la Posta, huku Hassan Sufiani akiuawa kwa kuchomwa na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali.

Mbuche Said naye alikutwa amepigwa na kisha kunyongwa katika chumba kimoja cha nyumba ya kulala wageni na kuna kijana mwingine aliuawa na kuporwa pikipiki.

"Nimempigia simu Waziri wa Mambo ya Ndani, Masauni nimemwambia Kilindi tunakufa aongeze nguvu ya wataalamu kukabiliana na mauaji haya yanayotutia hofu wananchi," amesema Makengwa

Mwindad Salum ambaye ni dereva bodaboda mjini Songe amesema mwenzao Abdallah alikodishwa na mwananmke aliyekuwa amevaa mavazi ya kufunika uso, alipomchukua hakurudi tena hadi tulipokwenda kuokota mwili wake jana, tumevunjika nguvu hata ya kufanya hii kazi ya bodaboda," amesema Mwindad.

Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na mauaji hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa amesema vyombo vya dola vimeanza kuwasaka wanaoendesha matukio hayo ya mauaji na kuwaomba wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kuwafichua wauaji hao.

"Niwatoe hofu wananchi wenzangu wa Songe na Kilindi kwa ujumla,vyombo vya dola vipo kazini,tutawakamata wote ili kuhakikisha Kilindi inaendelea kuwa salama," amesema Mgandilwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Camachius Mchunguzi amesema tayari kuna watu wanashikiliwa kuhusiana na matukio hayo na kwamba jeshi lilo litahakikisha kinawanasa wote walio katika mtandao huo wa mauaji.