Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania 940,507 wapata chanjo ya Uviko-19

Watanzania 940,507 wapata chanjo ya Uviko-19

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Jumla ya Watanzania 940,507, tayari wamepata chanjo ya Uviko-19, sawa na asilimia 88.9 ya mzigo wa chanjo uliopokelewa awali.


Moshi. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Watanzania 940,507  tayari wamepata chanjo ya Uviko-19, sawa na asilimia 88.9 ya  chanjo zilizopokelewa awali.

Hayo ameyasema leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya Yubile ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini (KCMC).

"Hadi kufikia Oktoba 15, 2021 jumla ya Watanzania 940, 507 wamechanja, sawa na asilimia 88.9 ya mzigo wa chanjo tulioupokea awali, niwahakikishie wananchi, Serikali inaendelea kuwezesha upatikanaji wa chanjo," amesema Rais Samia.

"Niwakumbushe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19, sina haja ya kusema mengi hapa Moshi, takwimu tulizonazo zinaonyesha jinsi Moshi ilivyoathirika na ugonjwa huu.

"Niwahimize wananchi kuchanja na kuchukua tahadhari zote kujiepusha na athari kubwa za ugonjwa huu, kwani kwa mujibu wa wataalamu hili ugonjwa bado lipo na hatujui lini litatoweka kabisa ulimwenguni," amesema.

Awali akiongoza ibada ya shukrani  ya Yubile ya miaka 50, Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika  kupambana na ugonjwa wa Uviko- 19 ambao umekuwa ni janga la dunia.

" Rais wetu na mama Yetu Samia Suluhu Hassan tunakushukuru na kukuunga mkono mia kwa mia katika kipindi hiki kwa namna unavyopambana na ugonjwa wa uviko 19 maana umekuwa mstari wa mbele," amesema Askofu Shoo.

"Nimehuzunika kusikia baadhi ya viongozi na hata wa dini kuhamasisha watu kutofuata taratibu za kujikinga na ugonjwa huu, Rais Samia Mungu amekuweka kipindi hiki kwa neema yake tunakushukuru na tunakuunga mkono," amesema Askofu Shoo.