Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania waitwa kongamano wabobezi wa AI duniani

Makamu Mwenyekiti wa ARIFA, Athuman Mfutakamba (Mwenye tai nyekundu), akizungumzia kongamano la Kimataifa la AI na Hatima ya Kazi (ICAFoW 2026)

Muktasari:

  • Katika kongamano hilo Watanzania wataonesha bunifu zao, uwezo wateknolojia pamoja na kufundishwa matumizi yake kwa kila mtu ikiwemo bodaboda, wauza vitumbua hadi mamalishe.

Dar es Salaam. Watanzania wameitwa kuonesha bidhaa zao za kiteknolojia, bunifu pamoja na kujifunza kuhusu akili unde (AI) katika kongamano la Kimataifa la AI na Hatima ya Kazi (ICAFoW 2026) litakalofanyika kuanzia Septemba 24–26, 2026 jijini Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo, kutakuwa na wajumbe zaidi ya 1,000 na wazungumzaji 100 kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya Afrika, Asia na Marekani wanaotarajiwa kujadili nafasi ya AI kazini pamoja na umuhimu wake kwenye sekta mbalimbali.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa AI ya Afrika (Arifa) linatajwa kunufaisha vijana wa Kitanzania watakopata nafasi ya kuonyesha bidhaa na uwezo wao teknolojia, bunifu, maarifa, fursa na matumizi yake katika elimu, afya, kilimo, sambamba na wajasiliamali kujifunza uwezo na msaada wa AI.

“Vijana watapata muda wa kuonyesha teknolojia na bidhaa zao, uwezo tunao katika eneo hili na lazima tutumie rasilimali watu na taarifa zetu kama Tanzania na Afrika kwa ujumla,” amesema Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Arifa, Dk Dennis Mwighusa jana  Jumatatu Juni 15, 2026.

Aidha, Kongamano hilo litatoa nafasi ya kipekee kwa watunga sera, viongozi wa sekta, watafiti, wabunifu, wajasiriamali, wawekezaji, na washirika wa maendeleo kuchunguza, kujadili, na kuweka mikakati ya jinsi AI inavyobadilisha uchumi na jamii kote Afrika na kwingineko.

Vilevile, ujumuishaji wa AI katika sekta mbalimbali, zikiwemo fedha, biashara ya reja reja, kilimo, huduma za afya, elimu, sheria, na nyinginezo ni miongoni mwa mada jadiliwa katika kongamano hilo.

Aidha, ufahamu unaotokana na data na maadili, ubunifu wa kiteknolojia na mifano halisi ya matumizi, sera, udhibiti, na utawala bora, uchumi wa fursa za muda mfupi, utofauti, na ujumuishi pamoja na kazi za mbali, usalama wa mtandao, na hatima ya kazi.

"AI inabadilisha kila sekta ya uchumi wetu, na Afrika haiwezi kumudu kuwa mtazamaji tu katika mabadiliko haya. Kupitia ICAFoW 2026, Arifa inalenga kuleta pamoja watu na mawazo yatakayosaidia bara letu kuongoza mabadiliko haya," amesema Dk Mwighusa.

Makamu Mwenyekiti wa Arifa, Athuman Mfutakamba amesema katika kongamano hilo watajikita katika umuhimu wa AI kwenye sekta za madini, elimu, takwimu, sheria, kilimo na uchukuzi.

“Teknolojia, uvumbuzi na ugunduzi katika kutatua matatizo ya nchi zetu, Afrika uwezo tunao tunaweza kuangalia ushirikiano wa kuwa na vituo vya taarifa miongoni mwa nchi na nchi,” amesema.

Akifafanua AI na nafasi za kazi Alfred Tembo kutoka Arifa amesema inaweza kutumika katika kuongeza faida ufanisi na kuzuia hasara kwa wafanyabiashara aidha kuboresha mfumo wa usomaji kwa wanafunzi kwa kuwaletea taarifa sahihi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Koncept Group, Dk Krantz Mwantepele amesema kwa sasa kila mtu anatakiwa kutmia AI haijalishi anafanya nini hata kama ni mama au baba lishe au muuza genge.

“AI inasaidia katika ufanisi wa kazi, inapunguza gharama, haichukui kazi za watu bali inapaswa kujifunza ili kuitumia kwa ufasaha,” amesema.