Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania watakiwa kuombea viongozi, Taifa

Askofu wa Kanisa la Philadelphia Miracle Temple Shinyanga, Baraka Laizer

Muktasari:

Askofu wa Kanisa la Filadelfia Miracle Temple, Baraka Laizer amewataka Watanzania kuwaombea viongozi na Taifa ili waweze kuwatumikia kwa kufuata miongozo na kudumisha amani.

Shinyanga. Askofu wa Kanisa la Filadelfia Miracle Temple, Baraka Laizer amewataka Watanzania kuombea viongozi na Taifa ili waweze kuwatumikia kwa kufuata miongozo na kudumisha amani.

Pia, amewataka Watanzania wamrudie Mungu na kuacha maovu, ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwalinda mwaka mzima ili aendelee kuwalinda na kuwabariki.

Askofu Laizer ametoa wito huo leo Jumamosi Januari Mosi, 2021 katika ibada ya mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa la Philadelfia Miracle Temple lililopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Amesema Watanzania wote hawana budi kumrudia Mungu, kushikamana na kuachana na matendo yaliyo maovu ili aendelee kuwalinda na kuwatendea mema kila wakati.

"Tukumbuke kuombea Taifa letu na viongozi wetu huku tukirudi miguuni kwa Mungu na kumshukuru kwa matendo makuu aliyotufanyia na kutusitahilisha katika maisha yetu na anakusudia kufanya mambo makubwa kwetu" amesema Laizer.

Askofu Laizer amesema neno la Mungu linasema shukuruni kwa kila jambo na Mungu anatafuta watu wenye moyo wa kushukuru, na shukurani inamgusa Mungu na anafanya tena mazuri kwa mwanadamu.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple wamesema wataendelea kuombea Taifa na viongozi.