Watatu wafariki kwenye mapigano ya wakulima na wafugaji

Watatu wafariki kwenye mapigano ya wakulima na wafugaji

Muktasari:

  • Watatu wafariki dunia kwenye mapigano ya wakulima na wafugaji huku watu zaidi ya 50 washiliwa na polisi.

Lindi. Watu watatu wamefariki dunia baada ya kutokea mapigano ya wakulima na wafungaji katika Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa.


Tukio hilo limetoka juzi majira ya saa saba mchana baada ya mkulima Chande Magoma kumkuta mfugaji shambani kwake akilisha ngo'mbe mahindi yake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutoa Kwa tukio hilo.


“Nikweli tuna tukio Kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa  watu wawili, mkulima na mfugaji walipigana wakajeruliana  hadi kupelekea vifo vyao wote wawili.”


“Leo (jana) asubuhi kundi la wanakijiji wakalipiza kisasi kwa kumuua kijana mmoja ambaye waliamini anatoka kwenye jamii ya wafugaji, tuna washikilia watuhumia zaidi ya hamsini  kuhusiana na  matukio hayo, hata hivyo kuna utulivu, baada ya viongozi ngazi ya mkoa na wilaya kufanya mkutano na wananchi,” alisema Kitinkwi.