Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumishi NSSF Mufindi watakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa

Mufindi. watumishi wa mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF) Wilaya ya Mufindi wametakiwa kujiepusha na kuacha mara Moja vitendo vinavyoashiria masuala ya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Akizingumnza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa  wateja, ofisini hapo Meneje wa NSSF wilayani hapa,  Ngussa Somolo amesema kuwa endapo mtumishi ambaye anabainika amejihusisha na vitendo hivyo vya Rushwa  hawatakuwa na huruma kwa yeyote atakayehusika na vitendo hivyo.

"Ninawasisitiza watumishi wote kuwa rushwa ina madhara makubwa katika mfuko wetu na ni adui wa haki kwa sababu inaharibu sifa nzuri ya mfuko ambayo imejengwa mwa muda mrefu," amesema Somola.

Meneja huyo amesema kuwa mbali na suala hilo lakini pia kama mfuko wamejipanga kuhakikisha huduma zinaboreshwa na kuweka mazingira mazuri ya utoaji wa huduma huku akisisitiza watumishi hao kutimiza majukumu ya ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya wateje wao.

"Katika kuadhimisha wiki hii napenda kuwafamisha wanachama wetu kuwa tunatambua umuhimu wa mchango wao kwenye mfuko kwa sababu bila wao hakuna uendelevu wa mfuko huo," amesema meneja huyo.

Mmoja wa wanachama wa mfuko huo Wilayani hapa, Msiba Kyando amesema kwa sasa huduma za mfuko huo zimeboresha na zinatolewa vizuri huku akiwasisitiza wananchi wengine kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo.

"Niwasisitize wananchi wenzangu kujiunga na mfuko wa NSSF kwa sababu kwa sasa huduma zake nyingi zimeboresha na unaweza kupata huduma bila changamoto yoyote," amesema Kyando.