Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumishi wawili wanaodaiwa kuisababishia hasara MSD ya Sh14 bilioni 'wamuangukia DPP'

Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) na Halmashauri wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 37 yakiwamo ya wizi wa dawa na vifaa tiba wakiwa watumishi

Dar es Salaam. Mhasibu Mwandamizi wa Bohari ya Dawa (MSD), Suddi Abas (34) na Mfamasia wa Wilaya ya Singida, Wema Mohamed (39) wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania (DPP), wakiomba kukiri mashtaka yao na kuimaliza kesi hiyo.

Wakili wa washtakiwa hao, Method Kagoma, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu Aprili 27, 2026 wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Sudi mkazi wa Kibamba Shule na Mohamed mkazi wa Mandewa wilayani Singida, pamoja na wenzao wanne wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 7833 ya mwaka 2026 mahakamani hapo.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 37 yakiwamo ya wizi wa dawa na vifaatiba vyenye thamani ya Sh5.537 bilioni, mali ya MSD pamoja na kuisababishia hasara ya Sh14.6 bilioni.

Wakili Kagoma amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya kuwa wateja wake hao wawili wameandika barua kwa DPP wakiomba kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi hiyo.

"Mheshimiwa hakimu wateja wangu, mshtakiwa wa kwanza katika kesi hii (Suddi) na mshtakiwa wa sita (Wema) wamemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) wakiomba kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi hii," amedai Wakili Kagoma na kuongeza.

"Barua hiyo wameandika Aprili 20, 2026 kwenda Magereza na tayari imepokelewa Aprili 22, 2026," amedai wakili Kagoma.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Monica Ndekidemi, amedai kesi hiyo imeitwa kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika, hivyo wanaomba Mahakama iwapangie tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Sudd na Wema, washtakiwa wengine ni Petro Mdegela(42), Rashid Hassan(34), Edward Tengulaga(40) na  Jackson Mahagi(39) ambao wote ni wafamasia.

Hakimu Lyamuya baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 11, 2026 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wote wako rumande kutokana na mashtaka ya kutakatisha fedha yanayomkabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, leo washtakiwa hao hawakupelekwa mahakamani badala yake kesi hiyo imesikilizwa kwa njia ya mtandao.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Aprili 13, 2026 na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Kati ya mashtaka 37 yanayowakabili washtakiwa hao, mashtaka 31 ni ya kutakatisha fedha; matatu ni ya wizi wakiwa watumishi; mawili ni kuisababishia mamlaka hasara na moja ni kuongoza genge ma uhalifu.

Miongoni mwa mashtaka hayo, ni kuongoza genge, linalowakabili washtakiwa wote ambapo wanadaiwa kati ya Julai Mosi, 2021 na Juni 30, 2025 katika maeneo tofauti ya mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida na maeneo mengi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu kwa kutenda kosa la wizi wakiwa watumishi.

Shtaka la pili ni wizi wakiwa watumishi, linalomkabili Abas, Mdegela, Hassan na Tengulaga, wanaodaiwa kati ya Julai Mosi, 2021 na Juni 30, 2025 katika maeneo tofauti ya mkoa wa Dar es Salaam na Mbeya, wakiwa watumushi kwa vyeo vyao, wanadaiwa kuiba dawa na vifaatiba yenye thamani ya Sh2.695 bilioni, mali ya MSD, iliyofika mikononi mwao wakiwa waajiriwa.

Shtaka la tatu ni wizi linalowakabili Mshtakiwa Abasi, Mdegela, Hassan na Mahagi, siku na maeneo hayo, washtakiwa wanadaiwa kuiba Sh2.592 bilioni, mali ya MSD iliyofika mikononi mwao wakiwa waajiriwa.

Shtaka la nne ni wizi wakiwa watumishi wa MSD linalomkabili Abas na Mohamed, ambapo wanadaiwa kati ya Januari 1, 2023 na Juni 30, 2025 katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam, Dodoma na Singida, kwa pamoja wanadaiwa kuiba Sh250 milioni, mali ya MSD.

Iliendelea kudaiwa mahakamani hapo, kuwa shtaka la tano ni kuisababishia mamlaka hasara, shtaka linalomkabili Abas pekee yake, anadaiwa kati ya Julai 1, 2021 na Juni 30, 2025  katika ofisi za MSD zilizopo Keko, Wilaya ya Temeke, mshtakiwa kwa makusudi aliisababishia MSD hasara ya Sh9.1bilioni.

Shtaka la sita ni kuisababishia mamlaka hiyo hasara linalowakabili washtakiwa wote, katika kipindi hicho na katika mikoa hiyo, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya Sh5.537bilioni.

Shtaka la saba ni kutakatisha fedha, linalowakabili washtakiwa wote, katika kipindi hicho, wanadaiwa kutakatisha Sh5,537 bilioni huku wakijua kuwa shtaka hilo ni kosa tangulizi la wizi akiwa mwajiriwa.