Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili kortini wakidaiwa kujipatia Sh55 milioni za kiwanja

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa lao, Juni 15, 2024 eneo la Kigogo, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Emmanuel Simkamba (40) na Mary Simkamba (60) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka moja la kujipatia Sh55 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Juni 10, 2026 na kusomewa shtaka lao na wakili wa Serikali, Erick Mabagala, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga.

Wakili Mabagala amedai washtakiwa walitenda kosa hilo Juni 15, 2024 eneo la Kigogo, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Ilidaiwa washtakiwa wakiwa eneo hilo walijipatia fedha hizo kutoka kwa Arbogast Lyimo kwa madai wangemuuzia kiwanja namba KND/KGG/MBY2/1, wakati wakijua ni uongo.

Ilidaiwa, kiwanja hicho kina kibali namba KND10134 mali ya Rhoda Mosses na Allen Mosses Sinkamba, huku wakijua si kweli.

Washtakiwa baada ya kusomwa shtaka hilo walikana na upande wa mashtaka walidai upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali.

Hakimu Mwankuga alitoa masharti ya dhamana ambayo ni kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja, atakayewasilisha mahakamani fedha taslimu Sh13.7 bilioni au hati ya mali isiyohamishika ya kiasi hicho cha fedha.

Washtakiwa wamekamilisha masharti ya dhamana na hivyo wapo nje kwa dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 16, 2026 kwa ajili ya kutajwa.