Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili kortini wakidaiwa kukutwa na bangi ‘supermarket’

Washtakiwa wanaodaiwa kusafirisha kilo 32 za bangi, katika duka la Village Super Market, wakiwa chini ya ulinzi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Muktasari:

  • Gordhan na Basit, wanadaiwa kutenda kosa hilo Juni 10, 2026, Mtaa wa Chole, katika duka la Village Super Market, lililopo Wilaya ya Kinondoni.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Dhirendra Gordhan, (43) na Syed Basit (43), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilo 32.99.

Gordhan, ambaye ni mkazi wa Kariakoo na Basit mkazi wa Msasani, wamefikishwa Mahakamani hapo leo Jumanne, Julai 28, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 16719 ya mwaka 2026.

Washtakiwa wamesomewa shtaka lao na wakili wa Serikali Cathbert Mbiling'i, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga.

Wakili Mbiling'i, alieleza washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo Juni 10, 2026, mtaa wa Chole, katika duka la Village Super Market.

Washtakiwa wanaodaiwa kusafirisha kilo 32 za bangi, katika duka la Village Super Market, wakiwa chini ya ulinzi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Ilidaiwa, washtakiwa wakiwa eneo hilo walikutwa wakisafirisha kilo 32.99 za Bangi.

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka lao, hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu.

Upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwamba waliomba tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu Kiswaga alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Agosti 11, 2026 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa walipeleka mahabusu kwa sababu kiasi hicho cha bangi kimezidi kilo 20, hivyo hawana dhamana kwa mujibu wa sheria.