Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili kortini wakidaiwa kumuua ‘house girl’

Muktasari:

  • Fredrick Godfrey Urassa (67) pamoja na Neema William Ayo (33) wakazi wa Kijiji cha Uswaa wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyakazi huyo wa kazi za ndani, Zuena Bitaliho Bihumo (14).

Hai. Watu wawili ambao ni wakazi wa kijiji cha Uswaa, Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro wamepandisha kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya msichana wa kazi za ndani 'house girl', Zuena Bihumo (14) mwenyeji wa mkoa wa Kigoma.

 Wawili hao ni Fredrick Urassa (67) na Neema Ayo (33), ambapo leo, Novemba 14, 2023; wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka la mauaji ya mfanyakazi huyo wa ndani.

Watu hao ambao ni wakazi wa Kijiji cha Uswaa wilayani humo, wamefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Jasmine Abdul na kusomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nkamba Mbosela.

Nkamba ameieleza mahakama hiyo kuwa tukio hilo la mauaji lilitokea Oktoba 23, mwaka huu, katika Kijiji cha Uswaa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 28, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena.

Oktoba 26, mwaka huu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa alitoa taarifa ya kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa msichana huyo alifariki kwa kipigo baada ya mwajiri wake kumchapa na kitu kinachodhaniwa ni fimbo hali iliyomsababishia majeraha ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha kifo chake.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya kutenda unyama huo waajiri wa binti huyo ambao ni mtu na mke wake, walimfikisha marehemu Hospitali ya Wilaya ya Hai kama mgonjwa huku wakitambua kuwa alikuwa ameishafariki muda mrefu.

"Tunamshikilia mtuhumiwa mmoja mwanaume (Jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha binti aitwaye Zuwena Bitaliho Bihumo (14) mfanyakazi wa ndani mwenyeji wa Kigoma," alisema Kamanda Maigwa na kuongeza kuwa

"Mtuhumiwa huyo na mke wake walikuwa wakimfanyia ukatili binti huyo kwa kumchapa na kitu kinachodhaniwa ni fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na na hivyo kumsababishia majeraha makubwa yanayodaiwa kuwa chanzo cha kifo cha msina huyo.