Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wadakwa wakisafirisha dhahabu vipande 28

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Juma Homera akizungumza na waandishi wa habari na kuonyesha vipande 28 vya madini ya dhahabu vilivyokamatwa vikisafirishwa huku watu wawili wakishikiliwa. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia Novemba 11,2023.  kufuatia kikosi kazi  cha madini Mkoa  kushirikiana na maofisa madini  kufuatilia na kubaini mtandao wa utoroshwaji .

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema Serikali iko kwenye mchakato wa kujenga kituo cha Kanda cha madini ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wanaokwepa kulipa kodi.

Homera amesema hayo leo Jumapili, Novemba 12, 2023 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na  kukamatwa kwa watu wawili (majina yamehifadhiwa) wakisafirisha vipande 28 vya madini ya dhahabu kilogramu 1.08373 vyenye thamani ya Sh142.2 milioni.

Amesema watuhumiwa hao wamekamtwa usiku wa kuamkia Novemba 11 mwaka huu majira ya saa 6 baada ya kikosi kazi cha madini kwa kushirikiana na maofisa madini mkoa kuwa katika oparesheni ya kukabiliana na mtandao huo.

“Ushirikiano wa kikosi kazi  maofisa madini mkoa ndio umefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ,huku akibainisha watafikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya uchunguzi kukamilika ”amesema Homera.

Amesema madini hayo yalikuwa yakisafishwa kwenye gari aina ya Toyota Mark X huku ikielezwa kusafirisha kwa wanunuzi mikoa mbalimbali.

“Kufuatia tukio hilo  Serikali imepata hasara Sh13.2 milioni ikiwepo mrabaha Sh 8.5 milioni , ukaguzi Sh1.4 milioni, kodi ya huduma Sh426,687 na kodi ya zuio Sh2.8 milioni,” amesema

Wakati huo huo ametaka kikosi kazi cha madini kuendelea kufanya kazi kwa weredi katika kukabiliana na matukio hayo na kuonya  wafanyabishara na wachimbaji wa madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani serikali haitawafumbia macho.


Mikakati ya Serikali

Homera amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini iko kwenye mchakato wa kujenga kituo cha madini Kanda ili kukabiliana na matukio ya utoroshwaji wa madini katika Wilaya ya kimadini ya Chunya na Mkoa wa Mbeya.

“Tunashukuru udhibiti na mikakati ya Wizara ya madini kwani kwa sasa matukio ya utoroshwaji wa madini yamepungua na mwaka huu  ni tukio la pili,”amesema

Kwa upande wake, Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Oscar Kilowa amesema wataendelea na kudhibiti wa utoroshwaji wa madini unaofanywa na wafanyabishara wasiokuwa waaminifu.

Amesema kuwa lengo ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wachimbaji ikiwepo uhakika wa masoko sambamba na uwazi wa uwekezaji ili watanzania waweze kunufaika.

“Watanzania wengi wanajihusisha na madini hatuoni sababu ya kurejea nyuma ambako tumetoka kukabiliana na vitendo vya usafirishaji wa madini  kinyume cha utaratibu na kanuni za kisheria,”amesema.