Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili watiwa hatiani kujifanya maofisa TISS

Muktasari:

  • Akitoa hukumu hiyo leo Mei 30, 2023, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka Mahakama hiyo imeridhika pasipo shaka yeyote kuwa washtakiwa hao wamefanya kosa hilo.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Joshua Kamalamo (37) na Yahaya Kapalatu (31) kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh3.9 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS).

 Akitoa hukumu hiyo leo Mei 30, 2023, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka Mahakama hiyo imeridhika pasipo shaka yeyote kuwa washtakiwa hao wamefanya kosa hilo.

Kwa mujibu wa Hakimu hyo, Mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo kwa kuzingatia kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza kwa upande wa mshtakiwa Kamalamo yupo kwenye matibabu ya macho itampa adhabu kwa kuzingatia sheria.

"Kama Mshtakiwa Kamalamo ameweza kwenda hadi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akijifanya wao ni maofisa wa TISS, ili iwe fundisho kwa wengine; lazima Mahakama hii itoe adhabu," alisema.

Kabate alisema mshtakiwa Kamalamo anakabiliwa na mashtaka mawili la kudanganya yenye ni TISS hivyo mahakama hiyo inamuhukumu kulipa faini ya Sh1.4 milioni au kwenda jela miaka miwili na shtaka la kujifanya yeye ni ofisa wa TISS anahumiwa kulipa faini ya Sh1.5 milioni au kwenda jela miaka miwili ambapo kifungo cha jela kinaenda kwa pamoja.

Alisema kwa upande wa mshtakiwa Kapalatu Mahakama hiyo imemuonea huruma kwa sababu alipigiwa simu na mshtakiwa Kamalamo akimuomba wakutane feri kivukoni ili amsindikize mahala fulani hivyo asingepigiwa asingeenda kwenye ofisi ya DPP.

Kutokana na hilo Mahakama hiyo inakuhukumu kulipa faini ya Sh1 milioni Kwa kosa la kujifanya maofisa TISS au kifungo cha miaka miwili jela.

Alisema mahakama hiyo imeamumua kumpa adhabu hiyo ili asirudie tena anapopigiwa simu na kuambiwa aende sehemu fulani anatakiwa kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamelipa faini hiyo wamekwepa kifungo cha miaka miwili.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 99/2021, ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo Juni 12, 2021 katika ofisi za DPP zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini hapa.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washitakiwa hao wakiwa katika ofisi hiyo, walijitambulisha kwa (DPP) Slyvester Mwakitalu na Naibu wake (DDPP) Joseph Pande kwamba wao ni maofisa wa TISS, wakati wakijua kuwa ni uongo.