Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya 'Maofisa usalama feki' kuanza kusikilizwa April 21, 2022

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  •  Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga April 21, 2022 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS) inayomkabili mfanyabiashara Joshua  Kamalamo(37) na mwenzake Yahaya Kapalatu(31).

  


 Dar es Salaam. Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga April 21, 2022 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS) inayomkabili mfanyabiashara Joshua  Kamalamo(37) na mwenzake Yahaya Kapalatu(31).

Kamalamo na Kapalatu wanadaiwa kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu na Naibu wake Joseph Pande kuwa ni wao ni maofisa wa usalama wa Taifa( TISS) wakati wakijua ni uongo.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati shauri hilo lilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi.

Kabla ya kupangwa kwa tarehe hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga amedai kuwa shauri hilo limepelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikiliza, lakini hakimu anayesikiliza shauri Hilo, Godfrey Isaya yupo nje ya ofisi kikazi.

" Kutokana na sababu hiyo, tunaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza ushahidi" amedai Wakili Mwanga.

Wakili Mwanga baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 21, 2022 itakapoanza kusikilizwa.

Washtakiwa wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo kila mshtakiwa alipaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watakao saini bondi ya Sh7 milioni.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanakabiliwa na kesi ya  jinai namba 99/2021, ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo Juni 12, 2021 katika ofisi za DPP zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani, jiji hapa.