Waziri Dk Ndumbaro atangaza kiama kwa wasomi wanaotajwa migogoro ya ardhi

Waziri wa Katiba na sheria, Dk Damas Ndumbaro akizungumza na wananchi mkoani Kagera kwenye uwanja wa Mayunga Manispaa ya Bukoba kuhusu jinsi walivyojipanga kutatua migogoro na kesi kwenye jamii.
Muktasari:
- Amesema wizara ya katiba na sheria imejipanga kutokomeza migogoro ya ardhi, mirathi na ndoa ukatili wa kijinsia na ipo taarifa za migogoro na kesi nyingi na kusababishwa na baadhi ya wasomi kama maprofesa na madaktari kuwakandamiza wananchi wa kipato cha chini.
Bukoba. Waziri wa katiba na sheria Dk Damas Ndumbaro ametangaza kiama kwa baadhi ya wasomi, maprofesa na madaktari wanaosababisha migogoro kwenye jamii hasa ile ya ardhi kuwakandamiza wananchi wa kipato cha chini kwenye jamii katika kesi zinazokuwa zikiwakabili.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu,14,2025 akiwa mkoani Kagera Dk Ndumbaro amesema wizara kupitia kampeni mbalimbali wamepita mikoa 24 wakisuluhisha na kutatua migogoro kwenye jamii huku wakijifunza zaidi ili watakapofika katika mkoa huo wajue jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo mara nyingi zinazosababishwa na maprofesa pamoja na madaktari.
"Kupitia kampeni zetu tulizofanya kwenye mikoa ya kutatua migogoro na kesi kwenye jamii, ikiwemo ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia tulikuwa tukijifunza endapo tukifika mkoa Kagera mkoa wenye wasomi wengi na maprofesa tutakabiliana vipi"
"Kwa mfano kule Kanyigo (Misenyi) kuna maprofesa wengi kama kuna migogoro sasa tuko tayari kwenda huko kuhakikisha wananchi wanapata Haki," amesema Dk Ndumbaro
Takwimu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera zinaonyesha uwepo mkubwa wa changamoto ya migogoro na kesi zinazohusu ardhi kwa wingi ambapo migogoro 200 kila wiki kuripotiwa kwenye mabaraza ya ardhi.
Mara nyingi zinaonyesha watu wenye kipato cha juu, wasomi maprofesa na madaktari wakiwafikisha kwenye mabaraza na mahakama wananchi wa kipato cha chini.
Aidha Dk Ndumbaro amewatahadharisha wanasiasa wenye tabia ya kutaka kuwa viongozi na kusababisha maandamano yasiyo na utaratibu wa kisheria na kikatiba kuwa wizara haitasita kuwachukulia hatua.
Amegusia wanasiasa hivi karibuni ambao hawana ni ya nzuri kwa wananchi waliyohusishwa kuandaa maandamano na kushawishi wananchi kutoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu mwezi octoba,2025 huku akitaja mihimili ya kutatua changamoto na kutangaza kuwa hili jambo lisifanyike kikatiba kuwa ni Serikali, Bunge na chama kilichopo madarakani.
"Wewe unaandaa maandamano na kuleta migomo kwa wananchi wewe ni nani "mimi kama waziri wa katiba na sheria ni jukumu langu kusimamia sheria na vifungu vyake hatuko tayari kuhatarisha matatizo kwenye nchi"
Kwa upande wa mkuu wa Kagera, Fatma Mwassa amesema taarifa za migogoro mara nyingi imewahusisha hadi viongozi wa serikali za mitaa katika mkoa huo kama vile wenye viti na watendaji.
Amesema mkoa wamejipanga vizuri kupitia wataalamu wa kisheria mwenyekiti au mtendaji na watumishi yeyote atakayebainika kwenye kesi au mgogoro hawatasita kuwavua vyeo na kuwachukulia hatua.
Hata hivyo Mkoa Kagera leo, Aprili 14,2025 imezinduliwa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia lengo ikiwa ni kutaka kuwasaidia wananchi kupata usawa na haki kwenye migogoro na kesi zinazowakabili bure.