Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Kombani afariki dunia

Marehemu Celina Kombani.

Muktasari:

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema Kombani alipelekwa nchini India wiki tatu zilizopita.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani amefariki dunia jana jioni katika hospitali ya Appolo nchini India, alikokwenda kwa matibabu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema Kombani alipelekwa nchini humo wiki tatu zilizopita.

“Ni Kweli amefariki dunia leo jioni (jana) ndiyo ninachoweza kusema kwa sasa,” alisema Dk Kashillilah kwa ujumbe mfupi bila kueleza waziri huyo alikuwa akisumbuliwa na nini.

Katika mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM, chama hicho kilimpitisha Kombani kuwa mgombea tena ubunge katika jimbo la Ulanga.

Waziri huyo alishiriki vikao vyote vya Bunge la Bajeti lililomalizika mwezi juzi mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2015/16.

Wasifu wa Celina Kombani

Celina Kombani  alizaliwa Juni 19, 1959.

Alisoma katika Shule ya Msingi Kwiro mwaka 1968-1975, Sekondari ya Kilakala 1975-1978 na baadaye katika Shule  ya Sekondari ya Wasichana Tabora kwa masomo ya juu 1979-1981.

Baada ya masomo ya elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe 1982-1885 na kati ya mwaka 1994-1995 alisomea shahada ya pili ya uongozi katika Chuo cha Mzumbe.

Kabla ya wadhifa wake wa sasa ndani ya utumishi, Kombani aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi) 2008-2010, Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri Tamisemi, Ofisa Utawala mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine,  Meneja wa Kiwanda cha ngozi Morogoro na ofisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.