Waziri Mkuu mstaafu atoa ujumbe kwa Watanzania

Waziri Mkuu mstaafu nchini Tanzania, Cleopa Msuya (kulia) akiwa na karani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake nyumbani kwake Usangi, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro

Muktasari:

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Cleopa Msuya amehesabiwa Sensa ya Watu na Makazi huku akitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kazi hiyo.

Mwanga. Waziri Mkuu mstaafu nchini Tanzania, Cleopa Msuya amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi ili kuipa Serikali nafasi ya kupanga shughuli zake za kimaendeleo.

 Msuya amesema hayo leo Jumanne, Agosti 23, 2022 wakati akihesabiwa nyumbani kwake Usangi, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.

"Sensa ya mwaka huu itatoa mahesabu ya kuwezesha Serikali yetu ya awamu ya sita kuonyesha ni nini watakachokifanya kwa siku zijazo ili kuboresha maisha ya Watanzania," amesema Msuya

"Hii ni kazi kubwa sana inalofanyika, tunaomba kila Mtanzania ashiriki na kutoa taarifa zake kwa usahihi na kikamilifu ili kuipa nafasi Serikali ya kupanga shughuli zake za maendeleo," amesema Msuya

Sensa ya watu na makazi itakuwa ya siku saba kuanzia leo Jumanne Agosti 23, 2022 kwa makarani kupita kuandikisha.