Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu ziarani Songwe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili mkoani Songwe kuanza ziara ya kikazi siku tatu, atapata nafasi ya kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

  

Songwe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili mkoani Songwe kuanza ziara ya kikazi siku tatu, atapata nafasi ya kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba ameongoza viongozi wa mkoa huu katika mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Songwe saa 3:30 asubuhi ambapo baada ya kuwasili ameondoka kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ambako atakagua na kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya wilaya na kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Mwambani na kisha baadaye atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Kesho Waziri Mkuu atakagua Kiwanda cha kukoboa kahawa cha GDM katika Halmashauri ya Wilaya Mbozi na baadaye ataelekea katika Wilaya ya Momba ambako atakagua ujenzi wa soko la kimataifa la mazao Kakozi na kisha atakwenda Halmashauri ya Mji Tunduma.

Baadhi ya wananchi wameuzungumzia ujio wa Waziri Mkuu kuwa ni fursa ambayo viongozi wao watawasilisha kero zinazowasumbua ikiwemo miundombinu mibovu ya Barabara, ukosefu wa maji, kero ya upatikanaji mbolea ya ruzuku na baadhi ya vijiji kukosa umeme.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Songwe, Radwello Mwampashe amesema atamweleza Waziri Mkuu kuhusu kero za Barabara ya Mbalizi Mkwajuni yenye urefu wa zaidi ya kilometa 100 ili ijengwe Kwa kiwango cha lami, Barabara ya Mlowo Kamsamba yenye urefu wa kilometa 130, kero nyingine ni upungufu wa maji Mji wa Tunduma, ombi la ujenzi wa stendi ya mkoa ya kisasa.