Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye mahitaji maalum wapata msaada wa mavazi, viatu

Askofu wa kanisa la Tree mission international mkoani Kagera Goerge Mbandwa akitoa msaada wa mavazi kwa watu wenye mahitaji maalum. Picha na Alodia Dominick

Muktasari:

  • Jamii imetakiwa kuwasaidia watu wasio na uwezo wa kumudu mahitaji yao ili kuleta upendo na kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Karagwe. Jamii imetakiwa kuwasaidia watu wasio na uwezo wa kumudu mahitaji yao ili kuleta upendo na kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Hayo yamesemwa jana Januari 18, 2023 na Askofu wa Kanisa la kimataifa la One Tree Mission (OMIC), Goerge Mbandwa lililopo kijiji cha Biyungu Wilaya ya Karagwe, wakati akitoa msaada wa mavazi kwa watu wenye ulemavu, wasiojiweza na watoto yatima wapatao 150, msaada wa nguo na viatu vya Sh1.5 milioni.

"Naomba watu wenye uwezo kifedha tujitoe katika kusaidia watu wenye mahitaji maalum siyo kwamba wanahitaji kuwa hivi walivyo ni kutokana na mazingira wanayoishi, walivyozaliwa na pengine familia zao, tunapojitoa kusaidia watu kama hawa Mwenyezi Mungu anatuongezea maradufu," amesema Mbandwa.

Amesema katika kanisa la Biyungu kuna kituo cha uamsho kinachoshirikisha waumini wa madhehebu mbalimbali, ambao hushiriki kujifunza neno la Mungu na kuifikia jamii katika kuwapa mahitaji ya lazima na wanapanga ndani ya mwaka huu kuanza maandalizi ya kujenga kituo cha watoto yatima.

Miongoni mwa wazee waliopata msaada wa mavazi, Bernadol Rwabusisi, ameshukuru kwa msaada huo akisema umekidhi mahitaji yake ya nguo wala viatu.

Naye Abson Project ambaye ni yatima amesema yeye kama kijana mahitaji yake ni kupatiwa elimu itakayomwezesha kutoka kimaisha.