Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye ulemavu wataka utoaji haki rafiki

Washiriki katika kikao cha wenye ulemavu na TLS

Muktasari:

  • Serikali imetaja mambo mawili kuwa kikwazo katika utoaji haki kwa kundi la watu wenye ulemavu.

Dodoma. Wadau wa masuala ya walemavu katika utoaji wa haki nchini, wametaja mambo mawili kuwa kikwazo kikubwa katika utoaji haki kwa kundi la watu wenye ulemavu.

Mambo hayo ni pamoja na kukosekana kwa miundombinu rafiki kwenye majengo ya vyombo vya utoaji haki, pamoja na ukosefu wa wakalimani wa lugha ya alama kwa ajili ya wasiosikia.

Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha kupitia ripoti inayoangazia changamoto za upatikanaji haki kwa watu wenye ulemavu katika vyombo vya utoaji haki.

Kikao hicho kiliandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa ajili ya kutafuta njia ya kuwakwamua wenye ulemavu ili waondokane na changamoto hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwalimu Enock Mbawa wa Sekondari ya Dodoma amesema watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na kero mbalimbali katika vyombo vya utoaji haki nchini licha ya kelele wanazoendelea kupaza.

Mbawa ambaye ni mlemavu wa macho, amesema vyombo vya utoaji haki nchini ikiwemo mahakama na polisi bado vina changamoto, kwani ikitokea mlemavu ana kesi na akakosa mtu wa kumsaidia kutafsiri mambo ya kimahakama, lazima ataachana na hiyo keshi hivyo kupoteza haki yake.

Kutokana na hali hiyo ameiomba Serikali kuwekeza nguvu kwenye miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika majengo yote yanayotumika kutoa haki.

“Lazima kuangalia katika vyombo vyetu vya utaoaji wa haki kama mahakama na polisi ili kuwepo na uwezekano wa namna ya kumsaidia kiziwi kupata nyaraka za kesi ambazo anaweza kuzielewa ili afuatilie haki yake, vinginevyo akiona hana anacho kielewa lazima atakata tamaa na kuachana na kesi hiyo,” amesema Mbawa. 

Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Watu wenye Ulemavu, Bruno Mwakibibi, amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia kero ambazo wanakumbana nazo walemavu katika kupata haki mbele ya vyombo hivyo.

Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Kati, Mary Munisi, amesema lengo ni kuisaidia Serikali kufanya maboresho katika sheria pamoja na sera mbalimbali ili kuwawezesha walemavu kufikiwa na huduma za vyombo vya utoaji haki nchini.

Amesema moja ya kazi ya TLS ni kuisaidia Serikali kama kutahitajika kufanya maboresho kwenye sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 basi yafanyike ili kuboresha mambo ambayo yameonekana vikwazo kwa upatikanaji haki kwenye kundi hilo.