Wizara ya Kilimo yatangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba ametangaza kuwa ofisi yake itahamia Dodoma wiki ijayo.

Muktasari:

  • Uamuzi huo umekuja baada ya Waziri Mkuu kutangaza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwamba ofisi yake itahamia Dodoma ifikapo Septemba na wizara nyingine zitamfuata.

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba ametangaza kuwa ofisi yake itahamia Dodoma wiki ijayo.

Uamuzi huo umekuja baada ya Waziri Mkuu kutangaza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwamba ofisi yake itahamia Dodoma ifikapo Septemba na wizara nyingine zitamfuata.

“Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhamia Dodoma kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Magufuli la kila wizara kuhamia makao makuu ya nchi, hivyo wiki ijayo wizara yangu inatarajia kuhamia Dodoma,” alisema Dk Tizeba jana alipokutana na wadau wa mifuko ya hifadhi za jamii na bandari kujadili uwekezaji katika uvuvi wa bahari kuu ili Serikali iweze kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo.

Akizungumza katika Siku ya Mashujaa juzi, mjini Dodoma, Rais Magufuli alisema lazima ofisi zote za Serikali zihamie Dodoma.