Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara ‘yawangáta sikio’ wachimbaji wadogo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo (wa kwanza kulia) akitoa maagizo kwa watendaji wa Stamico alipotembelea kituo cha mfano cha kuchenjua dhahabu cha Lwamgasa wilayani Geita. Picha na Rehema Matowo

Muktasari:

Kituo cha mfano cha Lwamgasa kina uwezo wa kuchenjua tani 120 za mchanga wa dhahabu kwa mwezi, kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha na mahitaji halisi ya wachimbaji; hali inayoilazimu Serikali kuanza mchakato wa kukipanua kwa kuongeza mtambo utakaochakata tani 100 za mchanga wa dhahabu kwa siku

Geita. Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Dhahabu wametakiwa kutumia vituo vya mfano vinavyojengwa na Serikali kujifunza namna bora ya uchimbaji, uchenjuaji na uongezaji wa thamani ya madini ili kuongeza tija katika shughuli zao.

Akizungumza na wadau wa sekta ya madini baada ya kutembelea na kukagua vituo vya mfano vya Lwamgasa na Katente vilivyoko mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amesema lengo la Serikali la kuanzisha vituo hivyo ni kuwajengea wachimbaji wadogo uwezo katika kuchimba, uchenjua na kuongeza thamani ya madini ili hatimaye wafikie uchimbaji wa kati na wakubwa.

Awali, Meneja Uchimbaji Mdogo kutoka Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Tuna Bandoma amepngeza mwamko wa wachimbaji wadogo wa kutumia vituo hivyo huku akifichua kwamba vituo vya mfano vya Lwamgasa na Katente tayari vimeelemewa na wateja kiasi cha huduma kutolewa kwa foleni.

“Kwa mfano, foleni ya wateja wanaohitaji huduma ya kujifunza katika kituo cha mfano cha Lwamgasa tayari imejaa hadi Mei, 2024; tayari Serikali imeanza kumtafuta mkandarasi kuongea uwezo wa mtambo ili ichakate tani 30 za mchanga wa dhahabu kwa siku badala ya uwezo wa tani tisa za sasa,’’ amesema Bandoma

Amesema mpango huo unaotarajiwa kukamilika mwaishoni mwa mwaka huu utapunguza foleni iliyopo sasa kwa zaidi ya asilimia 50.

Amesema kwa sasa, uwezo wa kituo hicho ni kuchenjua tani 120 za mchanga wa dhahabu kwa mwezi, kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha na mahitaji halisi, hali inayoilazimu Serikali kuanza mchakato wa kukipanua kwa kuongeza mtambo utakaochakata tani 100 za mchanga wa dhahabu kwa siku.

Msimamizi wa kituo cha mfano cha Lwamgasa, Victor Augustine amesema tangu kianzishwe mwaka 2020, kituo hicho kimechenjua tani 2, 970 za mchanga wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo zilizotoa zaidi ya 34.7 za dhahabu zenye thamani ya zaidi ya Sh4.3 bilioni.