Ujinga, uzembe unavyosababisha maradhi yanayoepukika

Muktasari:

  • Akiwa na miaka 45, akifanya kazi kama msimamizi wa kiwanda cha kupasua mbao kilichopo eneo la Buguruni Chama jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni vigumu kwangu kumtambua wakati nilipokutana naye akiwa katika kituo chake cha kazi.

Mara ya mwisho Gerald Zoka kupata maumivu ya kifua ilikuwa miaka mitano iliyopita na hakika ilimgharimu kwani alilazimika kutokwenda kazini kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akiwa na miaka 45, akifanya kazi kama msimamizi wa kiwanda cha kupasua mbao kilichopo eneo la Buguruni Chama jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni vigumu kwangu kumtambua wakati nilipokutana naye akiwa katika kituo chake cha kazi.

Akiwa ametapakaa vumbi mwili mzima huku mkono wake wa kulia ukiwa umeshika kipisi cha sigara Zoka analazimika kusafisha uso wake kwa mkono ili angalau nimwone na hatimaye nizungumze naye.

Wakati nikimkaribia ili nijitambulishe, chumba alichokuwemo kilikuwa kimetapakaa kwa vumbi la mbao na moshi wa sigara hali ambayo ilinifanya nibanwe na kifua na kuanza kupiga chafya. Mashine ya kusaga mbao pamoja na mtu aliyeitumia akiiendesha akiwa upande mmoja inaunguruma huku watu wawili wanayoendesha mashine hiyo wanapitisha magogo katikati yake.   

Baada ya kuisimamisha mashine hiyo, wanaanza kazi ya kuondosha msumeno ulionasiwa takataka za mbao. Siyo wakati wa kuiendesha mashine wala wanapoondosha msumeno huwa wamevalia vitendea kazi za kuwalinda na usalama wao.

Pia, wala hawajavaa glovu, vitu vya kujikinga masikioni wala kinga nyingine yoyote ya kujihadhari na vitu vyenye asili ya chupa na hawana viatu vigumu. Hivi ni vitu vya msingi ambavyo kwa kawaida mtu anayefanya shughuli ya namna hiyo anapaswa kuwa navyo kama sehemu ya kujikinga na majanga.

Kwa mara ya kwanza nilipomtembelea Zoka, rafiki yake wa karibu hakuwa amevalia kinyago. Hakuwa na chochote kwa ajili ya kulinda usalama wake. Hii ndiyo hali halisi inayoonyesha jinsi wasivyojali kuhusu usalama wa afya zao na ndiyo iliyomsababishia kukupata maumivu ya kifua wakati uliopita.

Huku akionyesha kinyago kilichotundikwa ukutani na vifaa vingine vya kulinda usalama, Zoka ananiambia kufanya kazi bila kujikinga na chochote ni jambo la muda tu.  “Najua ni hatari,” anasema Zoka huku akionyesha hali ya aibu, “ Tunajifanya tumesahau kuvitumia.”

Kimsingi anachokizungumza kinaaminisha maana nilipozunguka kutizama zaidi nilimwona akiwa amevivalia. Hata hivyo, wenzake hawakuvaa kabisa. 

Majanga yaliyoko nyuma yake

Kulingana na Dk Pauline Chale, ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya mapafu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kuna hatari nne ambazo zinaweza kumfanya mtu akumbwe zikihusishwa na vumbi.

Hatari hizo ni pamoja na kiwango cha vumbi kinachovutwa, ukubwa wake, aina na  matokeo ya kimwili wa mtu aliyeathirika.

Iwapo kiwango hicho ni kikubwa, ukubwa wake ni mdogo na aina yake ni sawa na mwili unategemewa kuathirika na hivyo kusababisha tatizo katika mfumo wa upumiaji kwa yoyote aliyekuwepo kwenye mazingira hayo.  

Dk Pauline anatolea mfano wa mtu anayefanya kazi kwenye kiwanda cha saruji huku akiwa hajajikinga kwa chochote. 

Vumbi la saruji anasema lina tabia kuwa la kawaida ambalo linaharibu mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kumweka mhusika katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mapafu.

Hali hii inajitokeza pia kwa watu wanaofanya kazi migodini na kwenye maeneo ya kupasua mbao au magogo.  

 Hakuna mbadala 

Buguruni Chama eneo ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa vifaa vya ujenzi na useremala siyo kawaida kuona mwendesha mashine akifanya kazi yake bila kuwa na kifaa cha kukinga pua.

Zoka sio mtu wa kipekee isipokuwa ndio utaratibu uliopo kwenye eneo hilo ambapo wafanyakazi wanashindwa kuona utofauti kati ya namna wanaojikinga na afya yao.

Unapouzungumza na baadhi ya wafanyakazi inaweza ikakuwia vigumu kuelewa ni kwa nini wamekuwa wakipuuzia kuvaa kinga licha ya ukweli kwamba baadhi ya wenzao wamekumbwa na matatizo ya kifua. 

Juma Ali mwenye miaka 32 ambaye ni msaidizi wa Zoka amekuwa akifanya kazi ya useremala kwa miaka mitano.

Rafiki yake Ali ambaye ni mpole na mwenye hali ya aibu ananieleza kuwa hajawahi kabisa kutumia kifaa cha kujikinga na madhara yoyote yanayoweza kuhatarisha afya yake akiwa kazini.

 Siyo kwamba vifaa hivyo havipo, bali anatoa sababu akisema kuvaa kifaa cha kukinga pua kinamfanya ajisikie akipumua vibaya.  

“Tangu siku hiyo nikacha kuvaa,” anasema licha kutambua namna anavyoiweka hatarini afya yake.

 

Watu kama wameziba masikio

Kwa ujumla hilo ndiyo jambo ambalo Dk Pauline amekuwa akikumbana nalo mara kwa mara toka kwa wagonjwa wake. 

“Watu” anashauri Dk Pauline katika mahojiano yaliyofanyika na gazeti hili hivi karibuni, “ wanahitaji kuwa waangalifu sana na afya zao na kuzingatia tahadhari za kiafya katika maeneo yao ya kazi,”.

Hata hivyo, ushauri kama huu hauzingatiwi na watu kama kina Ali ambao wanategemea kudura za Mungu kujikinga.

Kudhibitisha kuhusu nguvu za Mungu kulinda afya yake, Ali anasema amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka 15 na hajawahi kuugua.  Hata hivyo, bado hana uhakika kuhusu ujumla wa afya yake kwa vile hajawahi kwenda hospitalini kufanya vipimo.

Anasema iwapo itatokea siku moja ameathirika na vumbi kutokana na kazi yake, Ali ambaye ni baba wa mtoto moja anasema atahesabu tukio hilo ni kama ajali tu, “ kama ilivyo kwa ajali nyingine,” anasema huku akifurahi. 

Watu wamepoteza maisha kwa kupuzia

Bahati nzuri ni kwamba matukio kama haya hayajitokezi kwa wengine wanaofanya kazi zinazofanana nao kama vile wale wanaopaka rangi magari. 

Fredrick Mlaponi(25)anayefanya kazi ya kupaka rangi magari katika eneo la Buguruni Malapa anatambua fika kuwa anapaswa kuchukua tahadhari kwani bila kufanya hivyo anaweza kuitumbukiza hatarini afya yake.

Mlaponi anaufahamu wa kutosha kuhusiana na kemikali zinazopatikana katika rangi anazotumia kwenye magari.

Mbali ya kunywa maziwa kila wakati, Mlaponi na washirika wenzake wanne wamekuwa wakihakikisha wanatumia vifaa vya kukinga pua na maeneo mengine wakati wanapofanya kazi zao.

  “Kama msimamizi siwezi kuona mtu anafanya kazi bila kujilinda,” Mlaponi ananidhibitia kwa uhakika kabisa.

“Ni hatarini kupuuzia kutotumia vifaa vya kujikinga. Nimekuwa sehemu nyingi ambako watu wamepoteza maisha kutokana na kupuzia suala hili,”.

 

Afya zilivyo hatarini

Utafiti uliofanyika hivi karibuni uliyotathmini kuhusu dalili za matatizo yanayotokana na upumuaji na usalama wa kazi kwa mafundi seremala Dodoma ulionyesha kuwa vumbi zitokanazo na mbao husababisha kujitokeza kwa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa upumuaji.

Utafiti huo unataja maeneo matatu yanaongeza hatari ya kupata matatizo yanayoambatana na mfumo wa upumuaji. 

Maeneo hayo ni pamoja na kipindi gani mtu anaweza kudumu kwenye sekta ya ufundi seremala, kiwango, kwa kiasi gani anakumbwa na vumbi zitokanazo na mbao.

Kwa ujumla wafanyakazi wengi wako hatarini hasa kwa kuzingatia kuwa tafiti nyingi zinaonyesha kuwa Watanzania wengi bado hawalindi na kanuni za usalama sehemu za kazi na sheria zake.