Una ngozi iliyofubaa? fanya mazoezi haya

Muktasari:
- Mazoezi yanaifanya ngozi kuwa na afya njema kiasi cha kumfanya mzee wa miaka 50 kuonekana ni kijana huku yule ambaye anafanya mazoezi kila mara mara akionekana kutozeeka.
Inawezekana ulikuwa hujui kuwa mazoezi ni zaidi ya kipodozi chochote katika kukufanya kuonekana kijana mwenye ngozi ng’avu yenye afya na kustahimili mashabulizi ya vimelea.
Mazoezi yanaifanya ngozi kuwa na afya njema kiasi cha kumfanya mzee wa miaka 50 kuonekana ni kijana huku yule ambaye anafanya mazoezi kila mara mara akionekana kutozeeka.
Mazoezi mepesi yanayojulikana kitabibu kama Aerobics ndiyo ambayo yanayochoma mafuta yaliyorundikana maeneo mbalimbali mwili.
Wakati wa mazoezi viungo vya mwili ikiwamo misuli hufanya kazi ili kufanya mambo mbalimbali wakati wa mazoezi ndipo misuli hiyo huvunja vunja sukari (glucose) ambalo moja ya zao ni joto.
Joto la ndani linapopanda na kuwa juu mwili hujibu mapigo ili kuhakikisha kuna joto la wastani hivyo huupoza mwili na kulinda joto kwa kuruhusu jasho kutoka pamoja na joto.
Kipindi hiki ndicho ambacho jasho lenye taka mwili hutoka pamoja na joto ili kuupoza mwili, wakati wakufanya hivi ndipo ngozi kusafishwa.
Kitendo hiki huwa na faida sana kwa mwili kwa kuwa hata yale mafuta yanayorundikana chini ya ngozi pamoja na taka zingine huondolewa kwa kiwango kikubwa kipitia vitundu vya jasho.
Vile vile mazoezi haya wakati jasho linapotoka huweza kuondoa na vitu vingine ambavyo ni sumu na hata kuuwa vijidudu vinavyoweza kudhuru ngozi.
Lakini kiafya inashauriwa ukimaliza mazoezi uoge ili kuondoa taka sumu ambazo zinaweza kunasa juu ya ngozi na kusababisha shambulizi katika katika ngozi.
Vile vile kuna vitu kama mafuta vilivyotoka na jasho kupitia vitundu vya jasho endapo usipooga huweza kurundikana na kuziba vitundu hivyo na kuibua maradhi ya ngozi.
Vitu hivi kama vingerundikana vingeliweza kuathiri afya ya ngozi ikiwamo mkereketo wa juu ya ngozi, chunusi, vipele na harara.
Wakati wa mazoezi hasaidia kuondoa makunyanzi kutokana na tishu za juu ya ngozi kujinyoosha na kutulia huifanya ngozi kuwa imara na hivyo kutopata makunyanzi yanayomfanya mtu kuwa mzee.
Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu