Punguza vyakula vya protini kukabili tatizo la figo

Muktasari:

Changamoto ya tatizo hili ni kuwa wagonjwa wengi huwa hawaonyeshi dalili na kusababisha mpaka tatizo linakuwa sugu ndipo mgonjwa huanza kuhangaika kupata matibabu


Tatizo la figo linaweza kumpata mtu yeyote,  lakini wenye ugonjwa wa kisukari na maradhi mengine yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo na shinikizo la damu wapo kwenye hatari mara mbili zaidi.

Changamoto ya tatizo hili ni kuwa wagonjwa wengi huwa hawaonyeshi dalili na kusababisha mpaka tatizo linakuwa sugu ndipo mgonjwa huanza kuhangaika kupata matibabu.

Kwa wenye tatizo la figo, wanashauri kuacha matumizi ya vyakula vyenye protini nyingi, kupunguza mafuta na kutibu anaemia, pia wanashauriwa kutumia dawa za kumfanya apate haja ndogo mara kwa mara, ili kupunguza mwili

Matumizi ya  dawa zenye asili ya chuma au sindano maalumu ya kuongeza chembechembe za damu zinasaidia kufanya tatizo hili lisiwe sugu.

Kwa wale ambao hawana tatizo la figo, wanaweza kuliepuka  kwa  kuacha kuvuta sigara, kuwa na uzito unaofaa, kufanya mazoezi na shughuli mbalimbali pamoja na kuacha au kujizuia kunywa pombe hasa pombe kali.

Zingatia ulaji wa vyakula bora na punguza chumvi na matumizi ya mafuta au vyakula vya mafuta kwa sababu ya kuzuia shinikizo la damu na kuvimba mwili. Usiongeze chumvi kwenye vyakula vilivyopakuliwa na jizuie kula vyakula vyenye chumvi nyingi.

Pia acha tabia ya kutumia dawa bila kupapata ushauri wa daktari, fanya vipimo vya figo angalau mara tatu kwa mwaka.

Mwandishi Lucy Johnbosco ni mshauri wa wagonjwa wa kisukari