Ulaji wa mchicha kutakukinga na kushambuliwa na maradhi

Muktasari:
- Hata hivyo, mboga za majani za kijani zote zina rutuba ya madini ya chuma, vitamini A na C, na zinatumika katika kupunguza uzito wa chakula, huondoa kalori na maji yaliyomo katika mboga hizo husaidia kutibu ukosefu wa choo.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Nottingham, unaeleza kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani husaidia afya ya ngozi kwa njia za asili.
Hata hivyo, mboga za majani za kijani zote zina rutuba ya madini ya chuma, vitamini A na C, na zinatumika katika kupunguza uzito wa chakula, huondoa kalori na maji yaliyomo katika mboga hizo husaidia kutibu ukosefu wa choo.
Miongoni mwa mboga hizo ni mchicha ambao una virutubisho muhimu katika mwili wa bindamu kwa kuufanya mwili kuwa imara na kupambana na maradhi mbalimbali.
Ulaji wa mchicha kila siku utakusaidia kuzuia maradhi mbalimbali yanayoshambulia mwili.
Maji ya mchicha ulioshemshwa yakitumika kila siku yanasaidia pia macho kuona vizuri huku juisi ya majani hayo hutibu ugonjwa wa mtoto wa jicho.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu zilizowahi kufanyika, zinabainisha kuwa mchicha unafaida nyingi, miongoni mwa faida hizo ni kutibu matatizo ya kuumwa mgongo, kusafisha njia ya mkojo, damu na unatibu maradhi ya figo.
Pia unatibu minyoo, baridi yabisi, tezi la shingo, homa, huongeza damu, unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi huku ukirutubisha uwezo wa kuona vizuri.
Hata hivyo, umakini unahitajika katika usafishaji wa mboga za majani hasa zenye majani mengi kwa sababu zina kiwango kikubwa cha uchafu na vijidudu, iwapo hazitasafishwa vizuri.
Pia ili kupata ubora wa mboga za majani, zinapaswa zitumike vizuri katika ubora wake kwa kuoshwa vizuri kabla ya kukatwa na zipikwe zikiwa zimefunikwa na mfuniko ili zisipoteze vitamin C.
(Hadija Jumanne)