Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usichokijua kuhusu ulaji wa maharage na faida zake mwilini

Dar es Salaam. Licha ya maharage kuwa ni miongoni mwa mboga zenye faida kubwa mwilini na hivyo kuwa muhimu kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya, wataalamu wanasema maharage lishe, ndio maharage mazuri kwa ustawi wa afya na mwili.

Maharage yana kiwango kikubwa cha protini. Mbali na kutumika kama mlo wa binadamu, majani yake hutumika pia kama chakula kwa binadamu na mifugo, huku nyuzi lishe zilizomo wenye maharage husaidia mwili kumeng’enya chakula vizuri.

Mtaalamu wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Wessy Meghji anasema Maharage lishe ni aina ya maharage ambayo yameongezwa madini ya chuma na zinki kwa wingi ili kufanya yawe na manufaa bora zaidi mwilini.

Meghji anasema maharage hayo hayana tofauti na maharage mengine katika kulima na hata katika kupika.

Hata hivyo, uanzishwaji wake ni moja ya mkakati wa kupunguza tatizo la upungufu wa madini ya chuma ambayo husaidia kutengeneza chembechembe nyekundu za damu.

Chembechembe hizo za damu husaidia kuondoa tatizo la upungufu wa damu mwilini ambao huwapata zaidi wajawazito na watoto wadogo chini ya miaka mitano.

“Madini ya zinki yalipo katika maharage lishe husaidia ukujua wa watoto na kinga dhidi ya magonjwa kwa sababu hapa nchini kuna aina tatu za maharage ambazo tayari zimeshafanyiwa utafiti na kupitishwa” anasema Meghji.

Mtaalamu huyo anasisitiza wananchi watumie maharage lishe ili waweze kupata manufaa ya ukuaji wa afya ya mwili na akili.

Hata hivyo, maharage kiwango kikubwa cha protini ambavyo ni muhimu katika kujenga mwili wa binadamu na kwa msingi huo yanafaa kuwa mbadala wa nyama, maziwa, mayai au samaki.

Vile vile husaidia kukinga kiwango cha sukari kwenye damu kuongezeka ghafla baada ya mlo, hivyo ni muhimu kwa watu wenye kisukari au wanaoelekea kupata tatizo hilo.

Kama hiyo haitoshi, virutubisho vilivyomo katika maharage vinamwezesha mlaji kukabiliana na maradhi mbalimbali yanayotokana na upungufu wa protini au madini ya chuma na zinki.

Hata hivyo, ukosefu wa madini ya chuma mwilini huchangia mtu kupata maradhi yanayosababishwa na upungufu wa damu na upungufu wa nguvu mwilini.

Kama ulikuwa hujui, protini inayopatikana katika maharage husaidia katika kujenga mwili lakini maharage hayo pia yana vitamini B ambayo inasaidia kutengeneza seli za mwili.