Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ali Kiba: Atoboa kuhusu 'mapenzi' na Lulu,ugomvi na Diamond-2

Muktasari:

  • Baadhi ya mambo hayo ni madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Elizabeth Michael(Lulu). Pia kuwapo kwa taarifa za kusaini mkataba mkubwa na Kampuni ya Sony Music Africa iliyopo nchini Afrika Kusini.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Salehe Kiba maarufu Alikiba, amezungumzia yaliyomsibu hata kujiweka kando ya shughuli za muziki na ujio wake mpya.

Kiba alijiweka kando ya muziki kwa muda wa miaka mitatu, huku upande wa pili akikumbwa na skendo mbalimbali kuhusu maisha yake binafsi.

Baadhi ya mambo hayo ni madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Elizabeth Michael(Lulu). Pia kuwapo kwa taarifa za kusaini mkataba mkubwa na Kampuni ya Sony Music Africa iliyopo nchini Afrika Kusini.

Lakini kubwa ni madai kwamba kupotea kwa Kiba kumetokana na ujio na kukomaa kimuziki kwa msanii Naseeb Abdul (Diamond) na vilevile wakidaiwa pia kuwa na ugomvi uliokosa suluhu.

Gazeti hili lilimtafuta Kiba kutaka kujua mambo mbalimbali ikiwamo uhusiano wake na Diamond, ambapo katika gari yake msanii huyo alikutwa akisikiliza nyimbo za msanii Diamond Plutnumz, ‘Mawazo’.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa msanii huyo Kunduchi Beach.

Mwandishi: Naona unasikiliza nyimbo za Diamond kwa hisia, vipi uhusiano wenu, inadaiwa mna ugomvi mkubwa, tatizo nini?

Ali Kiba: Bifu langu na Diamond limejengwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Sijawahi kumchukia, wala sidhani kama na yeye ilitokea kwake. Naona kuna wafuasi wangu na mashabiki  wanaozungumza hivyo kama maoni yao kwenye picha au matukio yanayowekwa katika vyombo vya habari.

Mwandishi: Unamwelezeaje Diamond?

Ali Kiba: Ni mwanamuziki aliyeifanya Tanzania ijivune kwa muziki mzuri. Lakini pia anajitahidi  kutafuta soko la muziki nje na kukuza muziki wetu kwa kuutangaza katika soko la kimataifa.

Nilipoishia mimi kwa wakati ule, yeye amekwenda mbele zaidi. Najivunia hilo, lakini ajue kwamba, nami ninarudi kwa kasi ya ajabu.

Mwandishi: Una bifu na chombo chochote cha habari?

Ali Kiba: Sina bifu na chombo chochote cha habari. Inadaiwa kwamba nina bifu na Clouds kwa mujibu wa watu tofauti, lakini nakanusha kuwapo kitu kama hicho. Nipo nao vizuri na mara kwa mara hukutana nao, hasa watangazaji katika mambo tofauti.

Mwandishi: Kwa nini hujaonekana kwa kipindi kirefu kwenye matamasha ya Fiesta, ambayo huandaliwa na Clouds?

Ali Kiba: Natamani kufanya ziara hizo, lakini kwa bahati mbaya sijawahi kupatana na waandaaji kiasi kiasi cha malipo. Hilo limenifanya nishindwe kuhudhuria matamasha hayo. Ni mwaka wa nne sasa.

Mwandishi: Tuambie dau la Ali Kiba kwa sasa ni shilingi ngapi ili asimame jukwaani?

Ali Kiba: Bila Sh8 milioni, Ali Kiba hajasimama jukwaani kwa matamasha ya ndani ya nchi. Nje ya nchi ni habari nyingine.

Mwandishi: Inadaiwa kwamba uliwahi kumchukua aliyekuwa mpenzi wa marehemu Kanumba, mwigizaji Lulu. Hili unalizungumziaje?

Ali Kiba: Jamani kwani Kanumba alikutwa na nani, si Lulu. Ingewezekana vipi mimi kuwa naye wakati ana mtu mwingine?

Kitu hicho sijawahi kufanya na sitarajii. Lulu namfahamu ni rafiki yangu wa kawaida tangu enzi hizo mpaka sasa. Sijawahi kufikiria wala kutoka naye kimapenzi.

Mwandishi: Nasikia unataka kuoa ni kweli?

Ali Kiba: Sina mchumba, sasa nitaoaje? Unajua hivi vitu vinahitaji umakini mkubwa, siyo kama vijana wengi wanavyochukulia.

Sina mchumba kama ilivyoelezwa, hata yule binti niliyepiga naye picha, si yeye. Wakati ukifika, nitatangaza kwani kuoa ni lazima katika kukamilisha ibada.

Mwandishi: Kuna taarifa kuwa umesaini mkataba na Kampuni ya Sony Music ni kweli, vipi kuhusu dili yako na Marekani nayo liliishia wapi?

Ali Kiba: Kuhusu mkataba na Sony mtafahamishwa siku za hivi karibuni. Hapo sasa utapata kujua kama ni kweli au ni kampuni nyingine, unapotaka kutengeneza kitu kizuri huchukua muda kwanza.

Kuhusu dili ya One 8 nchini Marekani, ilikuwa ya muda tu na haikuwa ya kudumu.

Mwandishi: Kuna wakati kulisikika taarifa kwamba umekamatwa uwanja wa ndege, ilikuwaje?

Ali Kiba: Niliwahi  kukamatwa uwanja wa ndege nikihisiwa nasafirisha dawa za kulevya. Nilipekuliwa sana Afrika Kusini. Hii inatokana na tabia ya baadhi ya wasanii kujihusisha na biashara hii inayochafua sifa tuliyonayo.

Mwandishi: Umewahi kufuatwa na wafanyabiashara wakubwa wakitaka usafirishe dawa za kulevya au kurubuniwa ili utumie dawa hizo?

Ali Kiba: Hapana, sijawahi kufuatwa na mtu hata kunishawishi nitumie ‘unga’.

Mwandishi: Unatumia ulevi gani?

Ali Kiba: Shisha peke yake, sinywi bia, mvinyo wala pombe kali. Bali ninakunywa soda pekee.

Mwandishi: Ratiba zako zikoje kwa saa 24?

Ali Kiba: Sina muda sahihi wa kuamka kwa sababu napenda kulala sana. Lakini hata nikiamka, lazima nifanye kwanza mazoezi, kisha nakunywa chai hata kama ni mchana.

Baada ya hapo, ratiba zangu huwa hazieleweki, kwani hubadilika kulingana na matukio ya siku mpaka jioni ninapolala.