Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo muhimu kuzingatia ili kuboresha mahusiano-2

Muktasari:

  • Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa mawasiliano yanayofanywa kwa njia ya maneno yaani verbal ni ya asilimia isiyozidi thelathini na tano tu, wakati mawasiliano yasiyotumia maneno yaani non-verbal huchukua asilimia zaidi ya sitini na tano.

Si mara zote mwenye hasira atakwambia kaa mbali na mimi leo nimekasirika sana, inabidi kama mko kwenye mahusiano ujue kumjua mwenzako jinsi anavyokuwa akiwa na hasira. Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa mawasiliano yanayofanywa kwa njia ya maneno yaani verbal ni ya asilimia isiyozidi thelathini na tano tu, wakati mawasiliano yasiyotumia maneno yaani non-verbal huchukua asilimia zaidi ya sitini na tano. Hii inatuonyesha kuwa kama wewe umekuwa ukitegemea tu kupata mawasiliano kwa kuambiwa au kusikia ukiambiwa basi umekuwa ukikosa mengi sana, sasa jifunze kuona visivyozungumzwa na kuelewa maana halisi ya vile vinavyozungumzwa maana mara nyingine kinachozungumzwa si kile kinachomaanishwa.

3. Unyenyekevu

Hapa tunamaanisha uwezo wa kushuka na kukubali madhaifu yako bila kung’ang’anizwa, au kuombwa ili unyenyekee. Hapa namaanisha kunyenyekea kusiko kwa hofu bali kunakosukumwa na pendo hata katika nyakati ambazo mazingira yanaonyesha kabisa kuwa haki iko upande wako. Ni vema kujua kuwa unyenyekevu ni adui mkubwa wa usawa wa kijinsia, unyenyekevu pia ni adui mkubwa wa mfumo dume. Hapa namaanisha kuwa katika kunyenyekea hatujiulizi kuwa nani wa kwanza kushuka, wala kama ni mwanaume basi hauanzi kufikiri akilini mwako kwamba anayestahili kunyenyekea kwanza ni mwanamke. Unyenyekevu unafanywa kuwa tabia ya kawaida kabisa baina ya wote waliopo katika mahusiano.

4. Kuwa mwelewa (understanding)

Usiwe wakati wote unajaribu kukwepa lawama. Usiwe wakati wote unajaribu kutafuta vigezo vya uthibitisho katika kila unaloelezwa au kuambiwa. Jaribu kuwa mwelewa na kukubali kwa hekima yale yanayo elezwa pasipo ubishi, lawama au manung’uniko.

5. Uwezo wa kusamehe na kukubali kusamehewa

Hiki ndicho kipimo pekee cha kukuwezesha kutofautisha penzi la kweli na lile la uongo. Kama hautaweza kusamehe, pasipokujali ni nini umefanyiwa basi kuna shida katika pendo hilo. Katika mahusiano kuna wale wanaojua kukumbuka makosa ya nyuma na kuyaorodhesha mara yule mtu anapohitaji msamaha. Kuna ambao hawayasemi uliyowakosea ila wanayaweka ndani mioyoni mwao na kuyawaza kila waendapo na kukuwekea vinyongo vya muda mrefu. Kuna wasiokubali kusamehe na pia kuna wasiokubali kusamehewa ambao hawaoni kuwa walichokifanya kinaweza kuwakwaza wengine na kwa hivyo hakuna haja ya kutaka radhi, hawa ni wagumu zaidi. Kumbuka tunaposamehe tunayapa nafasi mahusiano yetu kwenda hatua nyingine ndani zaidi. Tunapata nafasi ya kujuana mapungufu yetu ili kutafuta maboresho zaidi. Zipo athari nyingi sana za kibaiolojia, kisaikolojia na hata za kiroho za kushindwa kusamehe, Na hii inatupeleka kuuamini ukweli kwamba kusamehe si sana kwa faida ya anayesamehewa bali anayesamehe. “We forgive for our own benefits”

Mambo hatari kwa wanaoingia katika mahusiano

1. Usitegemee sana vigezo vya nje kama vile sura, mwendo, mavazi, umbile n.k.

2. Ingawa elimu ni msingi, ni hatari kuitegemea iwe ndio kipimo chako kwatika kumpata rafiki.

3. Usitegemee sana maoni ya watu wengine, kumbuka kila mtu ana hisia na matakwa yake.

4. Kujua maisha ya awali na mwenendo mzima wa mwenzako ni muhimu, mambo ya kabila na koo husika ni ya msingi pia ila yasiwe ndiyo taa ya kumulika njia zako.

5. Kamwe usichaguliwe, au kupendekezewa mchumba au mke na watu wengine, waweza kuja kuwalaumu hao baadaye. Ruhusu moyo wako uhusike zaidi.

6. Umri ni muhimu ila sio msingi wa kuchagua rafiki

7. Usitoe maamuzi kwa kuangalia upendo wa nje, maana huu una hisia nyingi zisizo rasmi kuliko upendo wa ndani. Ni rahisi mtu kuweza kuwa “msanii”. Wako wengi waliowahi kusema ndiyo kwa kudanganywa na upendo huu na leo majuto amefanyika mjukuu kwao.

Kumbuka!

1. Tafakari nini hatima ya mahusiano yenu; Je ni ili kujifurahisha tu? Je ni katika kutafuta msaada wa kimasomo? Je ni ili kuwa pamoja katika mitoko na starehe nyingine? Je ni marafiki tokea katika familia zenu? Je ni katika kumuandaa mwenza wa maisha? Wako ambao wamejikuta wakiingia katika mahusiano ya kimapenzi wakati siko walikokutazamia wakati wanaanza mahusiano hayo, ni vema mkijiuliza mapema ni wapi mnako taka kuelekea.

Msijikute mnafika msikokupanga na kuanza safari ya kurudi au kuvunja kilichoanza, hii kuwa yenye maumivu sana moyoni na mara nyingi huwa tayari imeshapoteza muda wa muhimu maishani usioweza kufidiwa kamwe.

Unafanya nini unapotaka kuoa au kuolewa

1. Tengeneza mahusiano mazuri na wengine wanaokuzunguka, panua wigo wa mahusiano kwa wengine si tu wa nyumbani kwako, kazini kwako, chuoni kwako au unakoabudu.

2. Jitahidi kupata muda mzuri wa kuwekeza katika urafiki na yule utakayempata, msikimbilie tu kwenye uchumba ukafurahishwa na kuitwa mchumba, wako waliowahi kuitwa wachumba lakini hawakuziona hizo ndoa na badala yake maumivu walioachiwa ni makubwa.

Kamwe usisahau ili huko kwenye ndoa kuwe salama na pema ni vema kupitia urafiki, uchumba na kuifikia ndoa, njia ya mkato yoyote itaweza kukufikisha ila tarajia kuwa itakugharimu sana baadaye.

3. Amua ni aina gani ya ndoa unahitaji kuwa nayo maishani. Mfano; ndoa ya Kikristo, Kiislamu, kisheria, kimila, au kuishi na mwenza tu kirejareja.

4. Fahamu mambo ya kimila au kiutamaduni yahusuyo ndoa baina yenu.

Msiishie kusema sisi hatuamini mambo ya mila na jadi, sisi tumeendelea, sisi ni wa kisasa zaidi, sisi ni wa dini zaidi; msije mkajikuta baadaye mnarudi kuwatafuta hao mliowaita wa zamani ili kuomba ushauri.

Yakupasa uoane na mtu wa namna gani?

1. Mtu unayeendana naye kihisia

2. Mtu ambaye unaweza kumkubali na unaweza kujivunia.

3. Mtu anayekuvutia kutokana na pendo sio kutokana rehema au fadhila

4. Mtu ambaye uko tayari kumfia

5. Mtu uliyeko tayari kujivunia wakati wowote na mahali popote

6. Mtu anayeweza kukufanya ujisikie na kujivunia jinsia uliyonayo

Kanuni

1. Tafuta, ila pima ushauri toka kwa wengine

2. Angalia mazingira na hali inayokuzunguka na ujiulize kama ukotayari kuingia katika mahusiano yanayo tazamiwa kuwa ndoa baadaye

3. Tumia pia akili yako ya kuzaliwa. (common sense)

4. Hakikisha mna vitu vya kufanana, kutofautiana sana huleta misuguano na maumivu ya moyo, ndoa ni kituo cha furaha sio cha masononeko.

Nawezaje kumtokea au kujiwakilisha kwa ninaye mpenda (Aproaching)

• Kuwa wazi na mkweli

• Lenga kusudi lako,

• Maanisha