Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanamke aliyejaribu kumtingisha Kagame

Muktasari:

  • Diana mwenye umri wa miaka 35 aliamua kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa Rwanda siku ambayo Rais wa sasa wa nchi hiyo alitangaza katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Wiki iliyopita Mamlaka za Rwanda zilimtia nguvuni Diana Shima Rwigara akituhumiwa kuhatarisha usalama na kughushi nyaraka. Kabla ya hapo aliwahi kukamatwa kwa makosa mengine. Mama yake na dada yake nao walikamatwa katika mkasa wa awali.

Diana mwenye umri wa miaka 35 aliamua kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa Rwanda siku ambayo Rais wa sasa wa nchi hiyo alitangaza katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Jeshi la polisi nchini humo liliandika katika mtandao wa Twitter kuwa wa Diana pamoja na familia yake walikamatwa baada ya kushindwa kuitikia wito wa polisi waliopewa siku kadhaa nyuma.

Diana na ndugu zake Anne Rwigara na Adeline Rwigara wanatuhumiwa kughushi nyaraka katika mchakato wa kutafuta wadhamini ili aweze kugombea urais katika uchaguzi uliomalizika miezi miwili iliyopita.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilimuondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ambao ulishuhudiwa Paul Kagame akiibuka na ushindi wa asilimia 98.8 kwa madai kuwa aliwasilisha majina ya watu waliokufa kama wadhamini wake wa kugombea kiti cha urais.

Akihojiwa na Kituo cha televisheni cha Marekani, CNN, kabla ya kujitosa katika uchaguzi Diana alisema anajua kitakachompata lakini haogopi tena.

“Fisi akikukimbiza muda mrefu uoga huwa unapotea,” alisema huku akikiri kuwa anaumizwa na hali ilivyo hasa ya watu kushindwa kuongea kwa uwazi kwa sababu ya hofu.

Hata hivyo Rwanda ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na wabunge wanawake zaidi ya asilimia 61.

Mwaka 2003, Alvera Mukabaramba alijaribu kugombea Urais lakini alijitoa na kuungana na Kagame. Mwaka 2010, Victorie Ingabire aliyekuwa akiishi Uholanzi alikwenda Rwanda kugombea Urais lakini aliingia matatizo baada ya kuzungumzia mauaji ya Kimbari na kudai kuwa aliyakana hivyo alihukumiwa kifungo cha miaka 15.

Lakini kilichomtia matatani ni kukumbushia uchunguzi wa kifo cha baba yake, Assinapol Rwigara kilichotokea mwaka juzi.

Pamoja na ushupavu wake Diane hajawahi kufurahi siasa au utajiri wa baba yake ambaye alionekana kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya jeshi, siasa na biashara za nchi hiyo.

Diana ni mfanyabiashara na mwanaharakati wa haki za wanawake aliyezaliwa mwaka 1981, Rwanda na kitaaluma ni mhasibu.

Alikuwa anaanza siasa

Diana anasema alikuwa ameanza siasa kwa moja kwa moja kugombea Urais na ajenda yake kubwa ikiwa ni kutoweka kwa watu kila mara.

Katika moja ya mahojiano aliyofanya alisema kinachomuumiza ni kuona ni rahisi nchini humo kumpata mbuzi aliyepotea kuliko binadamu.

Alisema amesukumwa kugombea kutokana na namna uhuru wa kutoa maoni unavyominywa na kwamba anajua vyema azma yake itamgharimu.

Picha zake za utupu

Siku moja baada ya kutangaza nia yake ya kuwania Urais, mitandaoni zilionekana picha zikimwonyesha akiwa kama alivyozaliwa huku amejipumzisha juu ya kochi.

Diana anazikana picha hizo akisema si za kwake ingawa zilitengenezwa kwa umahiri wa hali ya juu ili kumdhalilisha na kumpunguzia nguvu kutimiza azma yake.

“Baada ya kuona picha hazikufua dafu, yakafuata mengine mengi ikiwamo kudaia kutumia majina ya watu, sikudanganya katika hili kama inavyoelezwa,” anasema Diana.

Maisha yake yamesimama

Biashara za familia zinachunguzwa, akaunti zake benki zimezuiliwa na kila hatua anayopiga inafuatiliwa na mamlaka za nchi hiyo hiyo. Unaandika mtandao wa CNN.

Diana anasema kwa sababu hawezi kufanya chochote na hana tofauti na mtu aliyekatwa viungo vyote.

Mkurugenzi wa mamlaka ya mapato ya nchi hiyo, Richard Tusabe alikiri kuwa biashara ya tumbaku inayoendeshwa na familia hiyo inachunguzwa.

Alisema rekodi zinaonyesha kuwa kuna udanganyifu ulikuwa unafanyika ili kukwepa kodi na pia zipo kodi ambazo hawakuzilipa kwa miaka mitano.

Kifo cha baba yake

Diana anakitaja kifo cha kutatanisha cha baba yake kuwa moja ya sababu zilizomsukuma kuingia katika siasa.

Baba yake Assinapio Rwigara alifariki Julai, 2015 katika ajali ya gari. Katika ajali hiyo iliyohusisha lori na gari dogo alilokuwa akiendesha kugongana.

Familia ya Rwigara inasema isingewezekana ndugu yao afe kwani lori hilo liligonga upande wa abiria lakini cha kustaajabisha maiti ya ndugu yao ilikutwa imehaibika vibaya.

Diana anasema baba yake hakufa katika ajali hiyo isipokuwa polisi walimfunika uso na mfuniko wa plastiki ili akose hewa na kisha kumkatakata.

Alisema anamtaka Rais Kagame aanzishe upya uchunguzi wa kifo cha baba yake ili ukweli ujulikane.